Timu ya Mpira wa Miguu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita, hii leo itashuka dimbani katika Uwanja wa Shule ya Sekondari, Galanos kucheza na Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kwenye mwendelezo wa Michezo ya SHIMISEMITA, hatua ya Robo Fainali.

Mechi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia majira ya saa 9 mchana, ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Geita iliweza kufuzu hatua hiyo baada ya hapo jana, kuivurumisha Timu ya Halmashauri ya Mji, Ifakara kwa jumla ya mabao 4-0 kwenye hatua ya 16 Bora.

Mara baada ya mchezo huo, Kocha wa timu hiyo, Kadege Fred aliwapongeza wachezaji wake huku akiwasisistiza kuendelea kucheza kwa nidhamu na kujituma ili waweze kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

Kwa upande wa Mchezo wa Mpira wa Mikono (ME na KE) hatua ya 16 Bora, Halmashauri ya Wilaya ya Geita itachuana na timu ya Manispaa ya Temeke.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa