Mkuu wa Wilaya ya Geita Wilson Shimo ametoa wito wa kuitaka jamii kujifunza kusoma na kuandika huku akiwaagiza watendaji wa vijiji na kata kuanzisha mfumo wa elimu ya watu wazima ili kuisaidia jamii kupata taarifa mbalimbali zinazohusu maendeleo yao ya kiuchumi.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Shimo ametoa wito huo akiwa katika ziara ya ufuatiliaji wa mpango wa kunusuru kaya Maskini kipindi cha pili alipokuwa akizungumza na wanufaika wa Mpango huo katika vijiji vya Bugalama na Isamilo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita na kubaini kuwa wengi wao hawajui kusoma na kuandika.
Mkuu wa Wilaya akiwa na Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Geita amewataka wanufaika wa Mpango huo wa kunusuru kaya maskini kutumia vizuri fedha wanazopata kwa kufanya ujasiriamali, kilimo, na ufugaji ili mpango huo ulete tija kwenye jamii.
Naye Mratibu wa mpango wa TASAF katika Halmashauri ya wilaya ya Geita Gabriel Evarist amesema kuwa mpaka sasa wameshatekeleza awamu sita iliyoishia mwezi wa 10 na kwa sasa wanafanya uwasilishaji fedha kwenye kaya 7320 ambapo hivi karibu
Kwa upande wao baadhi ya wanufaika wa Mpango huo akiwemo Bw.Nestory Maridadi amesema kuwa mpango huo umemsaidia katika kukodi mashamba kwa ajili ya shughuli za kilimo ambapo pia Mkuu wa Wilaya ametembelea baadhi ya Miradi ya wanaufaika hao ikiwemo ufugaji wa nguruwe na kupongeza hatua wanazopiga wanufaika wa Mpango huo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa