Na: Hendrick Msangi
NYALWAZAJA MAY 20, 2024
“Ni muda wa Kubadilika,Miradi ikamilike ili wananchi wafurahie miradi ya maendeleo,” ameyasema hayo Mhe Hashim Abdallah Komba Mkuu wa Wilaya ya Geita alipotembelea kata ya Nyalwazaja Halmashauri ya Wilaya ya Geita ikiwa ni sehemu ya Ziara yake katika kukagua miradi na kusikiliza kero za wananchi.
Akikagua miradi mbalimbali katika vijiji vya Nyalwazaja, Nyabulolo na Bushishi na Lishe, Mhe Komba amepokea taarifa za miradi ambapo changamoto kubwa ikiwa ni ucheleweshaji wa vifaa vya ujenzi kutokufika kwa wakati na wakandarasi kutokuwa site kukamilisha miradi.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba ameiagiza Kampuni ya Gesap Engineering Group Ltd inayotekeleza miradi ya shule na zahanati katika kata Nyalwanzaja kuwa site muda wote ili kazi ikamilike kwa ubora unaotakiwa na kwa kuzingatia mkataba wake ili wananchi waweze kupata huduma katika vituo vya afya na shule ambazo wameanzisha kwa nguvu zao.
Diwani wa kata ya Nyalwazaja Mhe William Bucheyegi, amemuomba mkuu wa wilaya kuendelea kuweka msukumo ukamilishaji wa miradi ili kuwapunguzia wananchi wa kata hiyo adha ya kutembea umbali mrefu kupata huduma za afya.
Gesap Engineering Group Ltd ni Mkandarasi anayetekeleza miradi ya shule na zahanati katika kata hiyo ambapo ametakiwa kuwa site muda wote ili kazi ikamilike kwa ubora unaotakiwa na kwa kuzingatia mkataba wake ili wananchi waweze kupata huduma katika vituo vya afya na shule ambazo wameanzisha kwa nguvu zao.
Mhe Hashim Abdallah Komba amewataka Watumishi wa umma kuendelea kushuka chini kusikiliza kero za Wananchi na kuzitolea majibu ili Wananchi hao waendelee kuwa na imani na Serikali yao inayo ongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Komba ameendelea kuwasisitiza wakandarasi hao kuwa na kasi katika ukamilishwaji wa miradi na sio kufanya maigizo kwani wananchi wanahitaji huduma katika maeneo yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa