NYAMWILOLELWA
Na: Hendrick Msangi
NYABUSAKAMA ni Chama cha Ushirika kinachoundwa na muunganiko wa Vijiji Saba ambavyo ni Nyakabale, Nyansalwa, Nungwe, Bugulula, Saragulwa, Kasota na Manga chenye jumla ya wanachama 426.
Chama hicho kilianzishwa mwaka 2016 na kupata ufadhili kutoka Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) kwa kuwajengea maghala ya kuhifadhia mpunga na alizeti kutoka kwa wakulima Saragulwa na Kasota.
Akisoma taarifa ya Chama hicho mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba alipotembelea kiwanda hicho May 26, 2024, Mwenyekiti wa bodi ya chama hicho ndugu Sakumi Makungu amesema chama hicho kimewawezesha wakulima kutumia fursa zilizopo katika masoko ya mpunga na alizeti kwa kuzalisha mpunga na alizeti kwa kuzingatia kilimo cha kisasa.
Ghala lililojengwa na kampuni ya mgodi wa dhahabu ya Geita (GGML) kwa kiasi cha shilingi 658,000,000 lenye uwezo wa kuhifadhi gunia 30,000 za mpunga sawa na tani 2,700 kata ya Nyamwilolelwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Mradi huo unawanufaisha wakulima wa mpunga 1,653 kupitia chama cha Ushirika (AMCOS) ya Nyabusakama, wakulima wengine wa kijiji cha Saragulwa na vijiji jirani kwa kuhifadhi na kuongeza thamani.
Aidha ndg Sakumi amesema chama hicho kimeendelea kuongeza thamani ya mpunga na alizeti kwa kutumia kiwanda cha kisasa cha kukoboa, kugredi na kupaki mchele, pamoja na mashine ya kukamua mbegu za alizeti kupata mafuta safi ya alizeti na kuuza mazao yao kwa kuzingatia mbinu za ujasiliamali ili kuwa wakulima wafanyabiashara.
Wanachama hao wameiomba ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita kuwajengea uwezo wa kupata mkopo kwani mkopo walio nao kutoka benki una waumiza na kusema Bora waurudishe mkopo huo kwani kwao umekuwa changamoto.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba akiwa na baadhi ya wajumbe wa timu ya menejimenti Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakisikiliza namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi. Kiwanda hicho kina uwezo wa kukoboa tani 1.2 za mpunga kwa saa
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ndg Karia Rajabu Magaro amewataka wanachama hao kujiandikisha ili wanufaike na Mikopo inayotolewa na Halmashauri kwani haina riba.
Pamoja na hayo, wajumbe wa bodi ya chama hicho wameiomba ofisi ya Mkuu wa Wilaya iwasaidie ili wawe sehemu ya wasambazaji wa mchele kulisha mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML ) ili chama hicho kiendelee kukua.
Akiwa katika ghala hilo lililojengwa na kampuni ya mgodi wa dhahabu ya Geita (GGML) kwa kiasi cha shilingi 658,000,000 lenye uwezo wa kuhifadhi gunia 30,000 za mpunga sawa na tani 2,700 na kukoboa tani 1.2 za mpunga kwa saa, Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba ameipongeza bodi ya chama hicho cha Ushirika cha NYABUSAKAMA na kampuni ya mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) kwa uwekezaji huo na kukitaka chama hicho kuendelea kuwa wabunifu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ndg Karia Rajabu Magaro akiwa na wajumbe wa bodi ya Chama cha Ushirika cha Nyabusakama (AMCOS) ya Nyabusakama, AMCOS Ltd wakati alipotembelea Kiwanda hicho cha Kuchakata Mpunga na kuwashauri wakope mikopo isiyo na riba inayotelewa na serikali kupitia Halmashauri
“Mkawe na ushirika wa kisasa ili kuendelea kupata vyanzo vingine vya mapato katika kuendesha mradi kwa kuwa na miradi ya kujiongezea kipato kwa kuzalisha, kununua na kuuza badala ya kutegemea wanachama pekee” amesema Mhe Komba
Magunia ya Mpunga wa wanachama yakiwa yamehifadhiwa kwenye ghala hilo lenye uwezo wa kuhifadhi gunia 30,000 za mpunga sawa na tani 2,700. Mpaka sasa Idadi ya wanachama ni 426, wanaume wakiwa 313 na wanawake 113
Wajumbe wa bodi hiyo wamemshukuru Mhe Mkuu wa wilaya na timu ya menejemeneti ya Halmashauri ya wilaya ya Geita kwa kuwatembelea huku kauli mbiu yao ikisema Nyabusakama-Pamoja tujenge uchumi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa