Kuelekea mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mh. Hashim Komba ameagiza suala la Uwajibikaji kwa Wakuu wa Idara kwa kusimamia vikamilifu miradi ya kimaendeleo ili iweze kukamilika kwa wakati.
Akizungumza tarehe 9, Aprili wakati akifungua Kikao cha Kwanza cha kujadili maandalizi ya Mwenge wa Uhuru, 2025 katika Ukumbi wa EPZ-Bombambili, Halmashauri ya Manispaa Geita, Mh. Komba amesema kuwa Kila Mkuu wa Idara anapaswa kuwajibika na miradi iliyopo, na kujiridhisha kabla ya kupita kwa Mwenge wa Uhuru.
Katibu Tawala (W) Geita, Bi. Lucy Beda ameshauri suala la Hamasa kuelekea Mwenge wa Uhuru-2025, lifanyike mapema ili Wilaya ya Geita iweze kufanya vizuri.
Mratibu wa Mwenge wa Uhuru-2025 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Ndg. Alexander Herman akiwasilisha mapendekezo ya njia ya Mwenge utakapopita kukagua na kuibua miradi mbali mbali ya maendeleo.
Wajumbe kutoka Halmashauri ya Wilaya na Manispaa ya Geita wakifuatilia Kikao cha Kwanza cha Maandalizi ya Mwenge wa Uhuru-2025.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa