Baraza Maalum la Madiwani Halmashauri ya Wilaya Geita limeketi leo tarehe 27 Mei kujadili kuhusu mapendekezo yaliyotolewa katika uundwaji wa mkoa mpya wa Chato kuwa Wilaya mpya ya Busanda inayopendekezwa na hifadhi ya Taifa kisiwa cha Rubondo kuchukuliwa katika uanzishwaji wa mkoa huo mpya.
Kutokana na kuangalia sababu za kiuchumi, kijografia, na idadi ya watu na baraza hilo halijaridhia wilaya hiyo ya Busanda inayopendekezwa kuondolewa Mkoa wa Geita kwa sababu ndio eneo pekee linalotegemewa kwa mkoa wa Geita katika suala la mapato kutokana na uzalishaji mkubwa wa dhahabu.
Aidha Madiwani hao wameeleza kuwa Mkoa Geita hatakuwa na eneo jingine la utalii endapo hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Rubondo kikienda mkoa mpya wa Chato, hivyo haina budi kisiwa hicho kubaki kwa ajili ya utalii na kuongeza mapato kwa mkoa wa Geita.
Wilaya sita zinazopendekezwa kuanzishwa mkoa mpya wa Chato ni Bukombe, Chato, Ngara, Kakonko, Biharamulo, Wilaya mpya ya Busanda inayopendekezwa na kata tatu kutoka Wilaya ya Muleba.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa