Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Geita limepitisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya wajibu wa kampuni kwa jamii (CSR) kwa mwaka 2021 wenye jumla ya shilingi bilioni 4 na milioni 300.
Baraza hilo lililokutana hii leo Oktoba 5, katika mkutano maalumu wa baraza la Madiwani katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Nzera, limejadili mapendekezo ya Mpango huo na bajeti unaoonesha miradi yote iliyoanzishwa lakini bado haijakamilika.
Awali akiwasilisha mapendekezo ya mpango huo Mkuu wa Idara ya maendeleo ya jamii Bi.Furaha Chiwile alisema kuwa menejimenti imefanya tathmini kama ilivyoazimiwa na kikao cha kamati ya fedha, uongozi na mipango cha Agosti 9, 2021 na kubaini kuwa jumla ya miradi 1,251 iko katika hatua mbalimbali ikihitaji kiasi cha shilingi bilioni 15 na milioni 800 ili kuanza kutumika.
Ameendelea kusema kuwa kutokana na wingi wa miradi na gharama zinazohitajika ni dhahiri kuwa inahitajika zaidi ya miaka mitatu kuikamilisha miradi hiyo kwa kutawanya rasilimali kidogo kidogo kwa kila mradi, hali inayolazimu kuchagua miradi michache ambayo ikipewa fedha itaweza kukamilika na kuanza kutumika ili kudhihirisha dhana ya thamani ya fedha.
Ameendelea kusema kuwa kutokana na wingi wa miradi na gharama zinazohitajika ni dhahiri kuwa inahitajika zaidi ya miaka mitatu kuikamilisha miradi hiyo kwa kutawanya rasilimali kidogo kidogo kwa kila mradi, hali inayolazimu kuchagua miradi michache ambayo ikipewa fedha itaweza kukamilika na kuanza kutumika ili kudhihirisha dhana ya thamani ya fedha.
Aidha mpango uliopendekezwa na kupitishwa kwa mwaka huu 2021 unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 4 na milioni 300 ukiwa umezingatia maoni ya wadau na mapendekezo kutoka kwenye kata kwa kuhakikisha kwamba miradi itakayotengewa fedha inakamilika na kuanza kutumika.
Vigezo vingine ni pamoja na kuwa na uwiano kati ya miradi ya ujenzi wa miundombinu na huduma za jamii, miradi ya kiuchumi kwa ajili ya kuongeza kipato ili kupunguza umasikini wa kaya na kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama.
Aidha Miradi mingine ni pamoja na Afya bilioni 2 na milioni 114, Elimu msingi milioni 464, Elimu Sekondari milioni 256, Usimamizi na ufuatiliaji milioni 74, Utafiti na Maendeleo milioni 77 ambapo kwa ujumla inagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4 na milioni 300.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa