Kilele cha sikukuu ya wakulima nanenane kanda ya ziwa magharibi kimefanyika viwanja vya Nyamhongolo Mwanza na kuhudhuriwa na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Mwanza.
Kwa mahitaji ya mbegu za mazao na mifugo unaweza kutembelea ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Geita au Kuwasiliana kwa Simu +225 282520061 au Barua pepe: info@geitadc.go.tz
MAZAO NA MIFUGO
Zao la nanasi aina ya Smooth Cayene ambalo hukomaa ndani ya miezi 18 na kutoa mavuno tani 8 hadi 12 kwa mwaka. Halmashauri ya Wilaya ya Geita inalima kilimo cha nanasi kwa wingi hivyo wawekezaji wanakaribishwa kwa ajili ya kufanya uwekezaji katika zao hilo.
Kilimo cha zao la Mpunga aina ya TXD 306 (SARO 5) ambalo huchukua miezi 4 hadi kukomaa nakutoa mavuno tani 7-8.5 kwa ekari moja.
Kilimo cha zao la Muhogo aina ya Taricass 4 ambalo hukomaa ndani ya miezi 8-12 na kutoa mavuno tani 40-50 kwa hekta.
Zao la viazi lishe aina ya Blue 1 ambalo hukomaa miezi 3 hadi 4 na kutoa mavuno tani 4 kwa hekta.
Zao la alizeti aina ya HG 50745. Zao hili hukomaa miezi 3 hadi 4 na kutoa mavuno tani 2 hadi 3 kwa hekta.
Ufugaji wa Sungura. Wanyama hawa hutumika kama kitoweo vilevile mkojo wake husaidia kufukuza wadudu wasumbufu shambani/bustani.
Ufugaji wa Mbuzi wa maziwa aina ya Saanen na Toggenberg ambao hutoa maziwa lita 3-5 kwa siku, Bei ya mbuzi hawa huanzia kiasi cha shilingi milioni 1.5 na wanapatikana kata ya Bugulula kwenye kikundi cha wajasiriamali Nufaika.
Afisa Miradi kutoka kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Geita ndg Deogratius Ngotio akiwa na Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Geita (aliyevaa kofia) Wakati wa maonesho ya sikukuu ya wakulima nanenane viwanja vya Nyamhongolo Mwanza
Watumishi na wajasiriamali wakiwa wenye furaha baada ya kupokea kikombe cha ushindi nafasi ya tatu mamlaka ya serikali za mitaa katika viwanja vya maonesho ya kilimo Nyamhongolo Mwanza
Kilimo cha mbogamboga kinapatikana halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo wananchi hujishughulisha na kilimo cha mbogamboga kwa ajili ya chakula na biashara
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa