Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizosubiriwa kwa Hamu kubwa na wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita hatimaye zimefanyika siku ya Jana Septemba 01, 2025, Katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Mwenge wa Uhuru ulipokelewa alfajiri katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Lwezera. Hatua iliyofuata ni Mwenge wa Uhuru kupita katika Miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Serikali. Miradi iliyopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru ni pamoja na klabu ya Kuzuia na kupambana na Rushwa pamoja na klabu ya kupambana na madawa ya kulevya katika Shule ya Sekondari Bugando.
Mradi wa Barabara ya Kilometa 1.1 ya lami nyepesi katika Kata ya Nzera, Mradi wa ujenzi wa Wodi tatu katika Hospitali ya Wilaya Nzera, Ofisi ya kata ya Bugulula, Pia Mwenge wa Uhuru umetembelea na kujionea maendeleo ya shule ya sekondari ya Amali Chibingo iliyopo kata ya Nyamigota. Uzinduzi wa Mradi wa maji kijiji cha Inyala hatimaye Mwenge wa Uhuru ukatembelea kikundi cha vijana cha Katoro Terminal kinachojihusisha na kukodisha pikipiki za matairi matatu.
Katika Miradi yote hiyo Mwenge wa Uhuru Kupitia kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ismail Ali Ussi umempongeza mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Karia Magaro kwa usimamizi mzuri wa Miradi yote.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zinaendelea katika mkoa wa Geita zikiwa na Kauli mbiu isemayo Jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kwa amani na Utulivu.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa