Jumla ya watahiniwa 13,755 wa darasa la saba kutoka Halmashauri ya wilaya ya Geita wanatarajia kufanya mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi kwa siku mbili kuanzia kesho tarehe 05 na kumaliza tarehe 06 Septemba mwaka huu.
Akiongea mbele ya waandishi wa habari mwalimu Said J. Matiku Afisa elimu Msingi kutoka Halmashauri ya wilaya ya Geita amesema idadi hiyo inatokana na usajili wa watahiniwa uliyofanyika mapema mwaka huu ikiwa ni wavulana 6,713 na wasichana 7,042 na kati yao wanafunzi 12 ikiwa 9 ni wavulana na 3 ni wasichana kutoka katika shule za msingi 8 watafanya mitihani maalumu ya watu wenye uono hafifu.
Aidha kwa upande wa maandalizi yote yahusuyo mtihani huu kwa upande wa Halmashauri Matiku amesema “Maandalizi yote ya muhimu yamekamilika kwa asilimia themanini (80%) zilizobakia ishirini (20%)ni kwa ajili ya kusambaza mitihani kutoka makao makuu ya halmashauri na kupeleka kwenye vituo vyetu na kwa mwaka huu tuna vituo 32 vya kutunzia mitihani hiyo. Na nitumie nafasi hii kwa niaba ya menejimenti ya Halmasahuri ya wilaya ya Geita pamoja na watumishi wake kuwatakia mtihani mwema watahiniwa wote na Mungu awasimamie vyema ili wafaulu na kutimiza ndoto zao”.
Jumla ya shule za Msingi 176 zitashiriki mtihani huo ikiwa 174 ni mali ya serikali na shule 2 za Mawemeru na Wema zikiwa ni shule binafsi zinazofundisha kwa kutumia mchepuo wa Kiingereza.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa