Namna ya kujiunga na CHF
Unaweza kujiunga kama kaya,mtu binafsi au kikundi na kupatiwa kadi ya uanachama. Kila kaya(familia) itachangia kiasi kitakachokubaliwa kwa mwaka, mfano(5,000 au 10,000 au 15,000)
Mimi ni mwalimu wa shule ya msingi, je ninaweza kujiandikisha na familia yangu katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ?
Ndiyo, kama una wategemezi wa ziada ambao hawajasajiliwa katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Je wanafunzi wanaweza kujiunga?
Ndiyo, unaweza kuhudumia watoto katika familia,hii ikiwa ni watoto walioko katika kaya iliyojiandikisha ambao umri wao ni chini ya miaka 18.
Je naweza kujiunga kupitia kikundi cha uzalishaji au ushirika?
Ndiyo, unaweza ili mradi mkubaliane katika kikundi na uongozi wenu uwasiliane na Mganga Mkuu wa Wilaya au Mganga Mfawidhi wa kituo cha tiba kinachohudumia wanachama wa CHF kilicho karibu.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa