Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kuanza Agosti 2022 ili kuisaidia Serikali kupata takwimu sahihi na kuwahudumia watu wake kwa urahisi.
Akizungumza na wakazi wa mkoa wa Geita wakati akifungua maonesho ya 4 ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya madini Septemba 22 katika viwanja vya bombambili, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa Serikali inaweza kuwahudumia wananchi wake vizuri endapo itakuwa na takwimu sahihi za idadi ya watu wake,mifugo na masuala mengine.
Amesema kuwa zoezi la Sensa linasaidia Serikali kujua idadi ya watu na mahitaji yao hali inayosaidia pia kujua fedha hitajika za maendeleo katika maeneo hayo, sambamba na huduma za kijamii zinazotakiwa, huku akiwataka Viongozi mbalimbali kuendelea kuwaelimisha wananchi faida za sensa.
Sambamba na hayo Waziri Mkuu amewataka wananchi kuendelea kuomba kwa Mwenyezi Mungu na kufuata taratibu zote za afya zinazoshauriwa na wataalamu ili kujikinga na virusi vya korona, huku akisisitiza kuwa chanjo ni ya hiyari ila ni muhimu, kwa kuwa ina virutubisho vinavyoweza kumsaidia mtu ambaye hata ikitokea akaambukizwa virusi vya korona haathiriki sana kama ambaye hakuchanjwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa