Katika siku ya kwanza ya Utekelezaji wa zoezi la Chanjo ya Polio Halmashauri ya Wilaya ya Geita imefanikiwa kutoa Chanjo kwa watoto elfu 66 tofauti na elfu 44 idadi iliyokuwa imetegemewa awali kwa siku ya kwanza ikiwa ni mafaniko ya zaidi ya asilimia 100 katika utekelezaji wa zoezi hilo.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dr.Modest Buchard Lwakahemula (MD,MPH) ameeleza mafanikio hayo katika siku ya kwanza ya utekelezaji wa zoezi hilo lililoanza Mei 18 na kutarajiwa kukamilika Mei 21 mwaka huu.
Dr. Lwakahemula ametumia nafasi hiyo kutoa elimu kwa kusema kuwa ugonjwa wa Polio ni hatari na usio na tiba na endapo mtoto akiupata anaweza kudumu nao milele jambo ambalo ni hatari kwa familia, jamii, na hata taifa kwa ujumla kutokana na kulazimika kutumia rasilimali nyingi kumhudumia mgonjwa.
Aidha ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa ujumla na wadau mbalimbali ambao wameihamasisha jamii kujitokeza katika kufanikisha zoezi hilo hadi kuvuka malengo huku akiendelea kuwahamasisha ambao hawajijitokeza kutumia siku zilizobaki kupata huduma hiyo.
Kwa upande wake Msilanga Manyasi Mganga Mfawidhi zahanati ya Nyasembe na Timotheo Aloka Mganga Mfawidhi zahanati ya Inyala wamebainisha kuwa zoezi hilo linafanyika vizuri katika maeneo yao bila kukutana na changamoto kubwa na wameendelea kutoa elimu kwa wananchi wanaoonekana kuwa na mashaka juu chanjo hiyo.
Baadhi ya wananchi waliokuwa katika kituo cha kutolea chanjo katika zahanati ya Inyala akiwemo Bi.Mwaidi Athumani amesema kuwa amehamasika kuleta watoto wake kupata chanjo hiyo kwa hofu ya watoto hao kupoozaikiwa ni matokeo ya ugonjwa wa Polio.
Kampeni ya Kitaifa ya Ugonjwa wa Polio ambayo katika Mkoa wa Geita ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mh. Rosemary Senyamule Mei 18 mwaka huu kwa kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamalifu katika chanjo hiyo inayotolewa katika vituo mbalimbali vya huduma za Afya huku wataalamu wengine wakipita nyumba hadi nyumba kutoa chanjo hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa