Licha ya kukabiliwa na changamoto ya masoko ya kuuzia bidhaa zao, Kikundi cha Nguvu kazi kutoka Bukoli kinachofanya shughuli za ufinyazi, kimejipanga kushiriki kwa mara ya pili katika maonyesho ya Dhahabu yaliyoanza Septemba 16,2021 mkoani hapa.
Akizungumzia maandalizi ya maonyesho hayo mmoja wa wanakikundi hicho Bi.Tausi Rashid amesema kuwa,wanaendelea kuandaa bidhaa mbalimbali kwa ajili ya maonyesho hayo, ambapo baadhi ya vitu kama majagi,mitungi,vyungu na vyombo vingine viko katika hatua za mwisho za kukamilika.
Baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa na Kikundi cha Nguvu kazi kutoka Bukoli
Hata hivyo baada ya kueleza changamoto ya masoko ya kuuzia bidhaa zao ambazo kwa sasa wanatengenezea nyumbani na kuuzia minadani,Afisa biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bw. Jeremia Mgale, amewashauri kutafuta maeneo ya kuweka na kuuzia bidhaa zao, ili kuepuka changamoto ya kuhamishahamisha bidhaa hizo ambazo wakati mwingine zinavunjika.
Nguvu kazi ni kikundi chenye wanachama watano wanawake kutoka Bukoli ambacho kimeshawezeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Geita mara tatu,ambapo kwa mara ya kwanza kilipatiwa mkopo wa milioni 1 na kurejesha,kisha wakapatiwa tena milioni 2 na kurejesha,na hivi karibuni wamemaliza marejesho yao ya mkopo wao wa tatu wa milioni 5.
Afisa biashara kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bw. Jeremia Mgale akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanakikundi wa Nguvu kazi Bukoli alipowatembelea kujua muendelezo wa kazi zao.
Aidha wanawake hawa wana malengo ya kufanya vizuri zaidi kibiashara wakati na baada ya maonyesho ya Dhahabu, kwa kuwa uzoefu wao baada ya kushiriki katika maonyesho ya awali unaonesha biashara yao huwa inakua zaidi baada ya kujitangaza katika maonyesho.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa