Uongozi wa Bank ya Nmb Mkoani Geita , Oktoba 06,2025 umetembelea watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Makao Makuu ambapo Bank hiyo imeeleza mipango yake katika kushirikiana na watumishi kuchochea shughuli za maendeleo ndani ya Halmashauri na watumishi kwa ujumla.
Akizungumza katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ulipo Nzera, Meneja wa Bank hiyo Mkoani Geita Ndg Daniel Rauya amesema lengo la kukutana na watumishi wa Halmashauri ni kuendelea kutoka elimu ya Kifedha pamoja na nidhamu ya matumizi ya fedha pamoja na Huduma ambazo Bank ya Nmb inatoa kwa wananchi.
Naye Meneja Mwandamizi upande wa wateja binafsi wa Bank hiyo kutoka Makao Makuu Bi Beatrice Fussy ameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa namna ambavyo inatoa ushirikiano kwa Bank hiyo katika huduma za Kibenki
Akizungumza kuhusu CSR Maneja wa Bank hiyo Tawi la Geita Ndg Rauya amesema Bank ya Nmb ipo tayari kuchangia shughuli za maendeleo ndani ya Halmashauri ili kuendelea kuboresha huduma katika jamii.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dkt Alphonce Bagambabyaki ameushukuru Uongozi wa Benki hiyo kwa kuendelea kutoa elimu ya Kifedha kwa watumishi wa Halmashauri na kuwa tayari kuchangia shughuli za maendeleo huku akiwakaribisha kuendelea kufika mara kwa mara kutoa elimu.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa