Timu ya Menejimenti Halmashauri ya Wilaya ya Geita (CMT ) Oktoba 10,2025 imefanya ziara kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia fedha za Serikali Kuu na mapato ya ndani.
Katika ziara hiyo, jumla ya miradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.4 imetembelewa zikiwepo shule , Zahanati na vituo vya afya.
Wakizungumza kwa Nyakati tofauti Timu hiyo imewataka mafundi wanatekeleza miradi hiyo kuongeza kasi na kuzingatia ufanisi wa kazi ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na kuwahudumia wananchi.
Kwa upande wa wazabuni walioshinda tenda mbalimbali za usambazaji wa vifaa ujenzi wametakiwa kuhakikisha wanasambaza vifaa hivyo kwa wakati ili miradi hiyo ikamilike.
Pamoja na Maelekezo kwa mafundi na wazabuni, timu hiyo ya Menejimenti imewaelekeza wasimamizi wa miradi hiyo kutoa taarifa kwa wakati pale ambapo wanakutana na changamoto zinazopelekea kuchelewa kwa miradi.
Ufuatiliaji wa miradi ni sehemu ya mpango kazi wa Timu ya Menejimenti Halmashauri ya Wilaya ya Geita kuhakikisha miradi inakamilika kwa ufanisi ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa