Na. Agrey Singo.
Mwenge wa uhuru mwaka 2023 imepitisha miradi yote 11 yenye thamani ya shilingi 6,262,035,208 (bilioni 2.62) iliyotembelea na kukagua katika halmashauri ya wilaya ya Geita, Agosti 04, 2023.
Akizungumza katika katika uwanja wa shule ya msingi Ludete ambako mwenge wa uhuru ulilala mara baada ya kukamilisha kutembelea na kukagua miradi hiyo, kiongozi wa mbio hizo za mwenge kwa mwaka 2023 kitaifa, Ndugu Abdalla Shaib Kaim ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Geita kwa utekelezaji wa miradi hiyo kwa kukidhi viwango vinavyotakiwa na kuwa na nyaraka zote.
Baada ya kuwasili halmashauri ya wilaya ya Geita, mwenge wa uhuru ulitembelea na kukagua mradi wa sekta ya mazingira wa shamba la miti linalomilikiwa na Ndugu Paul Dennis Kamando katika kijiji cha Nyamilyango, mradi wenye thamani ya shilingi 23,340,000.
Aidha, mwenge wa uhuru ulikagua na kuzindua jingo la utawala katika shule ya sekondari Kasota, jingo lenye thamani ya shilingi 102,850,000 likijengwa na Mgodi wa Geita Gold Mine Limited (GGML) kama uwajibikaji wa kampuni kwa jamii (Corporate Social Responsibility- CSR).
Aidha, mwenge wa uhuru 2023, ulisimama na kutoa ujumbe wa mwenge kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi katika kijiji cha Saragulwa na kisha kwenda kugawa vyandarua 100 kwa wananchi katika zahanati ya Chigunga kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa malaria pamoja na kufanya usafi wa mazingira na upandaji miti katika zahanati hiyo.
Ukiwa katika shule ya sekondari Inyala, mwenge huo ulizindua klabu ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya sambamba na klabu ya kuzuia na kupambana na rushwa katika shule hiyo. Mwenge wa uhuru pia ukiwa katika kijiji hicho cha Inyala, uliweka jiwe la msingi katika mradi wa maji wenye thamani ya shilingi 463,975,432 unaotelekewa na Wakala wa Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA.
Pia, mwenge ulitembelea mradi wa kufuga kuku unaomilikiwa na kikundi cha kuku farm uliopo Nyamigota wenye thamani ya shilingi 6,000,000, kikundi hicho kimekopeshwa na halmashauri ya wilaya Geita kupitia kitengo cha maendeleo ya jamii.
Baada ya hapo mwenge wa uhuru 2023, ulitembelea, kukagua na kuweka jiwe la msingi katika Hospitali ya wilaya Katoro, mradi wenye thamani ya shilingi 3,200,000,000 ambapo kiongozi wa mwenge Ndugu Abdalla Shaib Kaim alotoa maelekezo machache ya kufanyia kazi kwa ajili ya kuboresha hospitali hiyo.
Mwenge wa uhuru ulimebelea na kukagua mradi wa ujenzi wa soko la kisasa Katoro, Mradi wenye thamani ya shilingi 1,889,669,776 unaotekelezwa na Mgodi wa Geita Gold Mine Limited (GGML) kama uwajibikaji wa kampuni kwa jamii (Corporate Social Responsibility- CSR) ambapo kiongozi wa mbio hizo za mwenge kwa mwaka 2023 kitaifa, Ndugu Abdalla Shaib Kaim alitoa maelekezo kwa ajili ya uboreshaji.
Mwenge wa uhuru mwaka wa 2023, ulitembelea, kukagua na kuzindua ofisi ya kata Ludete, mradi uliogharimu shilingi 68,000,000 ambapo baadaye ukamilizia kwa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya lami nyepesi CCM Katoro – Hospitali ya WIilaya kilomita 0.8 (mita 800) mradi unaotekelezwa na Wakala wa Barabara Vijijini Na Mijini- TARURA.
Baada ya mwenge kukamilisha shughuli ya kuembelea, kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi hiyo 11, akiwa katika uwanja wa shule ya msingi kiongozi wa mbio hizo za mwenge kwa mwaka 2023 kitaifa, Ndugu Abdalla Shaib Kaim aliipongeza halmashauri ya wilaya ya Geita kwa utekelezaji na usimamizi mzuri wa miradi yote ya maendeleo yanayotekelezwa, na kusema kuwa imekidhi viwango na nyaraka zote zilizotakiwa zilikwepo.
Kwa upande wake, mkuu wa wilaya ya Geita, Cornel Magembe aliwapongeza na kuwashukuru watumishi na wananchi wote wa halmashauri ya wilaya Geita wakiongozwa na mkurugenzi mtendaji Karia Magaro kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha katika kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa ufanisi mkubwa na viwango stahiki.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa