Na Hendrick Msangi.
Mkuu wa Wilaya ya Geita ndg Cornel Magembe amefanya kikao Shule ya Msingi Nyansalala iliyoko Kata ya Bukondo Halmashauri ya wilaya ya Geita kufuatia taarifa zilizo sambaa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha Walimu wa Shule hiyo wakiwa wamekalia vitabu baada ya Mtendaji wa Kijiji kuwanyang'anya Walimu hao madawati kwa madai Mkuu wa shule hiyo kuchelewesha kuleta samani hizo kama alivyo ahidi kwenye Vikao vya Kamati.
Hata hivyo jambo hilo limeshapatiwa majibu baada ya samani hizo kufikishwa katika shule hiyo na hii ni Kutokana na mzabuni aliyepewa kazi hiyo kutokukamilisha kwa Wakati kama ambavyo makubaliano yalifanyika katika Mkataba kati ya Shule na Mzabuni huyo.
Walimu wa Shule hiyo wanaendelea na majukumu yao.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi Kutoka Halmashauri ,walimu wa shule ya Msingi Nyansalala, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata hiyo, Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Geita, maafisa elimu Kata na Uongozi wa Serikali ya Kijijini.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa