Mwenge wa Uhuru ni chombo kilichoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zilianza rasmi mwaka 1964 baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwenge wa uhuru umekuwa kichocheo kikubwa katika kuimarisha uhuru wa Taifa letu,umoja wa kitaifa, kudumisha amani, kulinda Muungano na kuhamasisha maendeleo ndani na nje ya taifa la Tanzania.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg Godfrey Eliakimu Mnzava wakisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba kwenye viwanja vya mapokezi ya Mwenge kata ya Bugulula Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Itakumbukwa kuwa tangu mwaka 1964 hadi 1992, mbio za Mwenge wa Uhuru zilikuwa zikiratibiwa na kusimamiwa kitaifa na chama cha Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP) na baadaye Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya zake za Umoja wa Vijana.
Huu ni mwaka wa 32 tangu mbio za Mwenge wa Uhuru zirejeshwe chini ya uratibu na usimamizi wa Serikali ambapo kwa mwaka 2024 Mwenge wa uhuru umebeba kauli yenye kuwahamasisha wananchi kujitokeza kushiriki uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa amani na utulivu sambamba na kuendelea kushiriki kikamilifu katika harakati za kuhifadhi Mazingira kwa ujenzi endelevu wa Taifa chini ya kauli mbiu isemayo “Tunza mazingira nashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu”
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg Godfrey Eliakimu Mnzava akizindua Klabu ya kupinga na Kupambana na Rushwa shule ya sekondari Kasota
Aidha pamoja na kauli mbiu hii, Mbio za mwenge wa uhuru zitaendelea kuelimisha na kuihamasisha jamii ya watanzania kuhusu umuhimu na uzingatiaji wa lishe bora, mapambano dhidi ya rushwa, mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za Kulevya na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg Karia Rajab Magaro akipanda mti kwenye shambala Miti lenye ukubwa wa Ekari 6 linalomilikiwa na Ndg George Patrick Chomanga wakati wa mbio za mwenge wa Uhuru kama sehemu ya kuunga juhudi za Serikali katika utunzaji wa mazingira
Mwenge wa Uhuru 2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita umekimbizwa umbali wa 45.6 km kutoka eneo la Mapokezi hadi eneo la Mkesha na 30 km kutoka eneo la Mkesha hadi eneo la Makabidhiano hivyo kukimbizwa kwa jumla ya 75.6 km ambapo jumla ya miradi 14 yenye thamani ya jumla ya Tsh 2,898,164,073.58 inayohusisha miradi ya Maendeleo, Malaria, Lishe pamoja na Klabu za wapinga Rushwa na Madawa na Kulevya imetembelewa ikiwa ni pamoja Kuzindua, kuona,pamoja na kuweka mawe ya Msingi katika Miradi mbalimbali na baadaye kukabidhiwa Wilaya ya Sengerema Halmashauri ya Bushosa katika katika kijiji cha Nyamadoke Oktoba 6,2024.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg Godfrey Eliakimu Mnzava akipanda mti kwenye shambala Miti lenye ukubwa wa Ekari 6 linalomilikiwa na Ndg George Patrick Chomanga wakati wa mbio za mwenge wa Uhuru kama sehemu ya kuunga juhudi za Serikali katika utunzaji wa mazingira
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg Karia Rajab Magaro akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Geita (Kushoto) Yefred Miyenzi wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Oktoba 5, 2024 katika kata ya Bugulula
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa