Maeneo yenye shughuli za machimbo ya madini na uvuvi yatajwa kuwa hatarishi zaidi kwa maambukizi ya VVU katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Hayo yamebainishwa na Bi.Patricia Nsinde Mratibu wa UKIMWI katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita Disemba Mosi 2021, katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ambayo yalifanyika katika viwanja vya CCM Nkome katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Bi.Nsinde amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuna maambukizi zaidi katika maeneo ya machimbo ya madini, shughuli za uvuvi , vituo vya magari makubwa na katika shughuli za mikusanyiko ya watu hasa nyakati za usiku.
Aidha takwimu za kuanzia mwezi Januari hadi Oktoba 2021, kwa waliojitokeza kwa hiyari kupima VVU katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita zinaonyesha kuwa jumla ya watu 64,071 walijitokeza kupima VVU huku kati yao wanaume wakiwa 24,440 na wanawake wakiwa 36,631.
Aidha miongoni mwao ni watu 3,581 waliogundulika kuwa waathirika wa VVU ambapo wanaume wakiwa 1,491 na wanawake wakiwa 2,090 ambapo kiwango cha maambukizi kikiwa kimepanda kwa asilimia 5.9 ikilinganishwa na takwimu za mwaka jana 2020.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa