Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdor Mpango leo Februari 21,2025 amefunga Mkutano wa 109 wa wadau wa elimu kwa umma unaofanyika Jijini Mbeya.
Mkutano huo ulifunguliwa February 18,2025 na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Methusela Ntonda kwa niaba ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.
Akizungumza katika Mkutano huo Mhe Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango amewaeleza washitiri hao kuwa wao ni kiungo muhimu katika kuunganisha Serikali na wananchi kwa kuzitumia kalamu zao vizuri.
Vilevile Dkt Mpango amesema agenda ya matumizi ya nishati safi ni agenda ya Taifa kwani inatoa msukumo wa kuunga mkono mkakati wa Taifa unaolenga Asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ifikapo mwaka 2034.
Pamoja na hayo Dkt Mpango amesema Serikali imesaini makubaliano ya awali ya Kiasi cha Bilioni 8.4 na makampuni ya usambazaji wa nishati safi ili kupunguza gharama za matumizi ya nishati safi kwa wananchi katika kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi.
Aidha Dkt Mpango amewaeleza washitiri hao kuwa wanalo jukumu la kuhamasisha wananchi juu ya utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati safi.
Pamoja na hayo Dkt Mpango amewataka Maafisa Habari, Mahusiano na Mawasiliano kutoka Serikalini kuendelea kuwa daraja linaloiunganisha Serikali na wananchi kwa kutoa taarifa za mafanikio makubwa ya serikali.
" Nyie ni daraja linalounganisha serikali na wananchi hivyo mtoe taarifa kwa usahihi ziwafikie wananchi ili kuendelea kutunza amani na utulivu" Amesema Mhe Dkt Mpango.
Naye Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi amewataka Maafisa Habari na mahusiano na Mawasiliano kutoka Serikalini kuendelea kuyauza yale mazuri yote Serikalini inayoyatekeleza katika Taasisi zao.
" Serikali imeendelea kutekeleza miradi ya kimkakati ikiwepo Bwawa la Nyerere, Reli ya Kisasa (SGR), Daraja la Kigongo Busisi ambalo ni la sita kwa Urefu Afrika, pamoja na miradi mingine ya Maendeleo" Amesema Profesa Kabudi.
Aidha Profesa Kabudi ametoa wito kwa Taasisi mbalimbali kuendelea kulitumia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), kutangaza miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayub Rioba Chacha ametoa shukrani zake kwa Washitiri wa Mkutano huo na kusema jumla ya Washitiri 280 wamehudhuria Mkutano huo.
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwepo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Wakuu wa Mikoa ya Dodoma, Njombe, Songwe, Ruvuma, Wakuu wa Wilaya , Makatibu Tawala, Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali na viongozi wa Chama na Dini.
Mkutano wa 109 wa wadau wa elimu kwa umma umefungwa rasmi Februari 21,2025 huku ukibeba kauli mbiu isemayo Tumia Nishati Safi, Tunza Mazingira.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa