Kilele cha sikukuu ya wakulima nanenane kanda ya ziwa magharibi kimefanyika viwanja vya Nyamhongolo Mwanza na kuhudhuriwa na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Mwanza.
Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo chagua viongozi bora wa serikali za mtaa kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi yamefanyika kitaifa Mkoa wa Dodoma huku maeneo mengine yakiadhimishwa kikanda.
Wananachi wakiangalia bidhaa mbalimbali katika banda la maonesho sikukuu ya wakulima nanenane katika banda la Halmashauri ya wilaya ya Geita.
Aidha katika maonesho hayo Mkuu wa wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba ametembelea banda la Halmashauri ya Geita na kuangalia bidhaa mbalimbali ambazo zimewekwa kwa ajili ya maonesho zinapatikana Halmashauri ya Wilaya ya Geita ikiwemo kilimo cha nanasi, muhogo, mahindi, alizeti, viazi na mboga mboga.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Komba akiangalia bidhaa mbalimbali katika banda la maonesho sikukuu ya wakulima nanenane katika banda la Halmashauri ya wilaya ya Geita maonesho yaliyofanyika katika viwanja vya Nyamhongolo Mwanza
Pia Mhe Komba ametembelea wafugaji na wajasariamali wanaotengeneza mvinyo wa nanasi ambapo mbali na kusifu ubunifu mkubwa uliofanywa na kikundi hicho ameahidi kuwatembelea wajasiriamali hao ili kuona shughuli za uzalishaji unaofanywa na wajasiriamali hao.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg Karia Magaro akiwa ameshika Kombe la ushindi nafasi ya tatu kilichotolewa na mamlaka ya serikali za mitaa katika viwanja vya maonesho ya kilimo Nyamhongolo Mwanza. Wengine ni watumishi wa Halmashauri wakiwa na wajasiramali mbalimbali ndani ya Halmashauri katika kusherehekea ushindi huo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita imekabidhiwa cheti cha ushindi nafasi ya tatu mamlaka ya serikali za mitaa katika viwanja vya maonesho ya kilimo Nyamhongolo Mwanza
Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg Hendrick Msangi akiwa kwenye moja ya bustani ya mbogamboga katika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima nanenane.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa