Waganga Wafawidhi na Famasia wa vituo vya Afya,wametakiwa kuimarisha usimamizi wa dawa zinazopokelewa katika vituo vyao na kudhibiti mianya yote ya upotevu wa dawa.
Maazimio hayo yamefikiwa katika kikao cha timu ya Halmashauri ya Usimamizi wa Huduma za Afya (CHMT) na Waganga Wafawidhi, kilicholenga kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto mbalimbali za huduma za Afya.
Maazimio hayo yaliyoanza utekelezaji septemba 2,2021, yanawataka Waganga Wafawidhi na Mafamasia wa vituo vya Afya kuhakikisha kuwa, wanaohudumiwa dawa ni wale tu wanaostahili (CHF,NHIF,UF,EXEMPTION) ili kuondoa upatikanaji hafifu wa dawa muhimu kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya.
Aidha wakizungumzia changamoto ya makusanyo hafifu ya fedha za papo kwa papo (USER FEES),ikilinganishwa na huduma zinazotolewa kwenye vituo vya Afya, wamewataka Waganga Wafawidhi na Wahasibu wa vituo kuimarisha Usimamizi wa ukusanyaji wa fedha zinazopokelewa vituoni ili kudhibiti upotevu wa fedha na dawa.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa