Walimu pamoja na wenyeviti wa Michezo wa Tarafa nne zilizopo Halmashauri ya wilaya Geita, wametakiwa kufundisha na kuzingatia vipindi vya michezo shuleni ili wanafunzi waweze kufuzu mashindano yanayoandaliwa Katika ngazi mbalimbali za kitaifa na kimataifa.
Hayo yamesemwa na Afisa elimu msingi Halmashauri ya wilaya Geita Paul Magubiki alipokuwa mgeni rasmi kwenye Hafla fupi ya Kufunga mashindano ya UMITASHUMTA yaliyofanyika katika shule ya msingi Lutozo iliyopo Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro.
KATIKA mashindano hayo ya UMITASHUMTA kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, yaliyohusisha tarafa nne ya Bugando, Butundwe, kasamwa na Busanda, ambapo tarafa ya Butundwe imepata ushindi wa jumla kwa kupata makombe tisa (9).
Afisa Elimu, Magubiki amesema Michezo ni afya pia ni ajira, hivyo walimu wanapaswa kujifunza kwa tarafa ya Butundwe samabamba na kuwekeza katika michezo kwa Wanafunzi ili wanapoenda kwenye mashindano warudi na matokeo mazuri.
Akitoa taarifa ya UMITASHUMTA 2024, Afisa Michezo Halmashauri ya wilaya Geita Ibrahim Bunangoi amesema zaidi ya Wanafunzi 300 kutoka tarafa nne za Halmashauri ya Wilaya ya Geita, walikuwepo kwenye kambi ya mashindano na Wanafunzi mia Moja ishirini kati yao wamefuzu kwenda kwenye mashindano hayo ngazi ya mkoa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa tarafa ya Butundwe Renatus matogolo ambayo imepata ushindi wa jumla amesema siri ya ushindi wao ni kujituma huku Faida John mwenyekiti Bugando na Dominic Mabula mwenyekiti Busanda ambao tarafa zao hazikufanya vizuri sana, wamesema wataongeza juhudi zaidi ili wapate matokeo mazuri kwa wakati mwingine.
Kauli mbiu ya mashindano hayo ya UMITASHUMTA 2024 ni Miaka 50 ya UMITASHUMTA tunajivunia mafanikio katika sekta ya Elimu, Michezo, Sanaa hima mtanzania ushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa