Timu za Halmashauri ya Wilaya ya Geita zinazoshiriki michuano ya SHIMISEMITA 2025 jijini Tanga zimeanza kwa moto wa kuotea mbali baada ya kushinda michezo yote mitatu ya ufunguzi upande wa Netiboli, Mpira wa Wavu na Mpira wa Miguu.
Kikosi cha Mpira wa Miguu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita, kikiwa katika michuano dhidi ya Timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa.
Katika Mpira wa Wavu, Geita DC waliwachapa Ruangwa DC kwa Seti 2–0 bila huruma.
Katika Netiboli, ilikuwa maumivu kwa Moshi MC baada ya kupigwa 10–0 bila majibu.
Na kwenye Mpira wa Miguu, mabingwa watetezi Geita DC walionyesha makeke yao kwa kuilaza Kyerwa DC kwa mabao 3–0 katika dimba la Shule ya Sekondari Usagala.
Timu ya Mpira wa Pete kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Baada ya kipenga cha mwisho, Katibu wa timu, Timotheo Talai, alisema ushindi huo bado si kiwango halisi cha maandalizi ya Geita DC:
“Ni ushindi mdogo kwa jinsi tulivyojiandaa, lakini huu ni mwanzo tu. Mechi zinazofuata mtashuhudia ushindi mkubwa zaidi,” alisema kwa kujiamini.
Geita DC inaingia kwenye mashindano haya ikiwa ni bingwa mtetezi wa Mpira wa Miguu, baada ya mwaka jana kutwaa taji Mkoani Mwanza. Safari hii wamesisitiza hawapo Tanga kwa utalii, bali kwaajili ya kubeba vikombe na kuendelea kuandika historia. "Geita DC: Mbele, Mbele yao."
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa