Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim Komba, amefanya ukaguzi wa maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kuwasili Septemba 1, 2025. Katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya aliambatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Katibu Tawala wa Wilaya ya Geita Bi. Lucy Beda, pamoja na timu ya menejimenti kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba akiwa katika ukaguzi wa njia ya mwenge wa Uhuru 2025 unaotarajiwa kupokelewa Septemba 01, mwaka huu.
Ukaguzi huo ulianzia katika viwanja vya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru vilivyoko Shule ya Sekondari Lwezela. Aidha, ulijumuisha miradi mbalimbali ikiwemo Klabu ya Kupambana na Rushwa na Kupinga Madawa ya Kulevya katika Shule ya Sekondari Bugando, ujenzi wa barabara ya lami nyepesi yenye urefu wa kilomita 1.1 katika eneo la Nzera Centre, ujenzi wa wodi tatu katika Hospitali ya Wilaya ya Nzera, pamoja na Ofisi ya Kata ya Bugulula.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba katika picha na kamati ya usalama ya Wilaya, Timu ya menejimenti pamoja na wananchi katika zoezi la ukaguzi wa njia ya Mwenge wa Uhuru owaka 2025.
Miradi mingine iliyokaguliwa ni Shule ya Amali Chibingo, mradi wa maji Nyala, pamoja na kikundi cha vijana cha Katoro Terminal kinachojihusisha na shughuli za ukodishaji wa bajaji.
Baadhi ya mirada ya maendeleo inayotarajiwa kupitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025, katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Ziara hiyo imelenga kuhakikisha maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yamekamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyohitajika. Mwenge wa uhuru Mwaka huu una kauli mbiu isemayo, jitokeze kupita kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa Amani na utulivu.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa