Geita.
Kituo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) kimeendesha mafunzo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ya namna bora ya kuzitambua fursa za kibiashara na kuwekeza kwenye miradi ambayo itaweza kuchangia kwenye ukusanyaji wa mapato ya ziada kwenye Halmashauri.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ofisi ya Mkoa, Geita Aprili 10, yalilenga kuwajengea uwezo Maafisa wa Idara za Ardhi, Mipango, Biashara na Maendeleo ya Jamii, pamoja na kuonyesha umuhimu wa kutumia programu za PPP katika suala la utekelezaji wa Mipango ya Taifa ya Maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkufunzi kutoka PPPC, Dkt. Abiud Bongole, amesema kuwa, kutokana na ukuaji wa kasi wa Halmashauri mbali mbali nchini, ipo haja ya Wataalamu wa idara tofauti kuungana na kuona ni namna gani Halmashauri zitaweza kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato ili kusudi ziweze kujiendesha kwa ufanisi.
BUCKREEF KUGHARAMIA ZAIDI YA MILIONI 400 UTEKELEZAJI WA MIRADI.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa