Nzera-Geita
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe Charles Kazunguameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi na Menejimenti ya Halmashauri kwa usimamizimzuri wa miradi ya maendeleo wakati alipofanya ziara kutembelea na kukaguamiradi mbalimbali ndani ya Halmashauri.
Akizungumza katika Ziara iliyofanywa na Kamati ya Fedha, Uongozina Mipango kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Aprili 17,2025, MheKazungu ameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa namna inavyosimamia miradindani ya Halmashauri na kuwataka wahandisi wa Halmashauri kuendelea na kasikatika ukamilishaji wa Miradi.
" Kamati imeona namna ambavyo mnasimamia miradi, nitoe raikwenu kuendelea na kasi ili miradi ikamilike kwani nia ya Serikali nikukamilisha miradi wananchi wapate huduma" Amesema Mhe Kazungu.
Pamoja na hayo Kamati hiyo imeitaka Halmashauri kuona namna yaKujenga Ofisi za Watendaji za kisasa kwenye kila Kata ili kuendelea kutoahuduma kwa karibu kwa wananchi.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Kata ya Bugulula Bw. Juma Chomaameishukuru Ofisi ya Mkurugenzi kwa kutoa Kiasi cha Shilingi Milioni 70 kwaajili ya ujenzi wa Ofisi ya Mtendaji katika kijiji cha Kasota ambacho hadikukamilika kwake kitagharimu kiasi cha Shilingi Milioni 138.8.
Pamoja na hayo Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango iliwezakutembelea eneo la ekari 217 katika kijiji cha Sungusila ambalo Halmashauriinatarajia kulitwa kwa awamu ambapo kwa sasa katika eneo hilo jumla ya ekari 50zitatumika katika ukamilishaji wa majengo ya shule ya Amali iliyopo kata yaNzera.
Vilevile Kamati hiyo ilitembelea upanuzi wa Zahanati ya Nkome kuwakituo cha Afya mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Serikali kuu.
Ujenzi wa mradi wa upanuzi wa Zahanati ya Nkome kuwa kituo chaAfya unatekelezwa kupitia mpango wa Taifa wa Kuzuia vifo vya akina mama nawatoto (TIMCHIP) kwa gharama ya Shilingi Milioni 426.6.
Ziara hiyo ni sehemu ya Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango kukaguamara kwa mara miradi ya Maendeleo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita katikakuunga Juhudi za Serikali ya awamu ya Sita inayo ongozwa na Mhe Dkt SamiaSuluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya Maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa