Mradi wa maji ya bomba katika Halmashauri ya Wilaya Geita ulioghalimu zaidi ya Bilioni 4.9 umekamilika na wakazi wapatao 23,724 kutoka vijiji 5 vya Chankorongo, Chigunga, Chikobe na Kabugozo wameanza kutumia maji safi na salama
Ujenzi wa mradi huo ulioanza mwaka 2014 na kukamilika katika mwaka wa fedha 2018/2019 una mitambo 2 ambayo kila mmoja una uwezo wa kusukuma maji lita 155,000 kwa saa, matanki 4 ya kuhifadhi maji yenye ujazo wa lita 585,000, mtandao wa mabomba wa mita 56,800, nyumba 1 ya mhudumu wa mashine, vituo 54 vya kuchota maji pamoja na mabirika 8 ya kunyweshea mifugo.
Hata hivyo zaidi ya Bilioni 4.7 zilitengwa kwaajili ya kujenga miundombinu ya maji, milioni 237.8 kwa ajili ya miundombinu ya umeme na shilingi milioni 18.8 ni kwa ajili ya usimamizi wa ujenzi pamoja na uundaji wa jumuiya ya watumiaji maji COWSO.
Kukamilika kwa mradi wa maji Chankorongo kumesaidia kupunguza magonjwa yanayotokana na watu kutumia maji yasiyo salama, umbali wa watu kutafuta maji pamoja na kupunguza muda wa kutafuta maji, hivyo kuwezesha watu kupata muda wa kufanya kazi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa