Halmashauri ya Wilaya ya Geita Agosti 5, 2024 imeanza rasmi zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura ambapo linatarajiwa kukamilika Agosti 11, 2024.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 16 (5) cha sheria ya uchaguzi wa Raisi, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya mwaka 2024, uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura utakuwa mara mbili, kati ya kipindi kinachoanza mara baada ya uchaguzi mkuu na kabla ya siku ya uteuzi.
Afisa Mwandikishaji akiendelea na zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kata ya Nzera
Aidha, wanaohusika katika zoezi hili ni wananchi ambao wametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea, ambao hawakuandikishwa hapo awali, na watoto watakaotimiza miaka 18 kabla ya tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Wengine ambao wanaohusika na zoezi hili ni waliojiandikisha awali na wamehama kata au jimbo moja kwenda jingine, waliopoteza au kadi zao kuharibika, na wale ambao taarifa zao zilikosewa wakati wa uandikishaji.
Wananchi wakiwa katika kituo cha uandikishaji wadaftari la kudumu la mpiga kura
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji imeendelea na zoezi la uhamasishaji kwa kufanya matangazo sehemu tofauti ndani ya Halmashauri ili wananchi wajitokeze kuboresha taarifa zao katika vituo vilivyotengwa na baadaye waweze kushiriki zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa ifikapo mwezi Novemba kabla ya uchaguzi Mkuu utakao fanyika 2025.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa