Nzera-Geita
Timu iliyokuwa ikitekeleza Kampeni ya Msaada wa Kisheria ijulikanayo kama Mama Samia Legal Aid Compaign leo Februari 4,2025 imekabidhi repoti yake ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Kiongozi wa Timu hiyo kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi Scolastica Mality amesema timu hiyo imefanikiwa kwa asilimia 100 kwa kuzifikia kata 10 na vijiji 31 badala ya 30 vilivyopangwa
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dkt Modest Burchad akipokea taarifa ya Utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ijulikanayo kama Mama Samia Legal Aid kutoka kwa Mratibu wa Kampeni hiyo Bi Scolastica Mality
Kata zilizofikiwa ni Lwamgasa, Katoro, Ludete, Magenge, Kakubilo, Nyawilimilwa, Nkome, Bugulula, Isulwabutundwe na Nyarugusu ambapo jumla ya wananchi 30,954 wamefikiwa katika Kampeni hiyo na zaidi ya migogoro 81 imesikilizwa huku migogoro 10 ikitatuliwa hapo hapo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dkt Modest Burchad ameishukuru timu hiyo kwa kazi waliyoifanya na kusema Halmashauri itaendelea kutoa ushirikiano kila wakati.
Timu iliyokuwa ikitekeleza Kampeni ya Msaada wa Kisheria ijulikanayo kama Mama Samia Legal Aid Compaign ikiwa katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita kukabidhi taarifa za utekelezaji wa Kampeni hiyo
Timu hiyo ilianza utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria Januari 26,2025 na kuhitimisha Februari 4,2025.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa