Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kipindi cha miaka mitano (2020-2025), imefanikiwa kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo yenye thamani ya Tsh. 59,503,288,056.82.
Akisoma taarifa ya mafanikio yaliyoweza kupatikana ndani ya kipindi hicho, kwenye kikao maalumu cha tarehe 20, Juni, Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Ndg. Karia Magaro, amesema kuwa, miradi iliyoweza kukamilisha ndani ya kipindi hicho imejumuisha sekta ya Elimu, Afya, Utawala, Maendeleo ya Jamii, Kilimo, Uvuvi, Mifugo, Biashara, Miundombinu, Utamaduni, Sanaa na Michezo, pamoja na Mazingira.
Fedha hizo zimetokana na Mapato ya Ndani ambayo Halmashauri iliweza kukusanya ndani ya kipindi hicho, Ruzuku kutoka Serikali kuu, pamoja na Fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo.
Aidha, Halmashauri iliweza kupokea kiasi cha Tsh. 22,357,592,890.00 ikiwa ni fedha za Elimu bila malipo, zilizoelekezwa kwenye kuinua Elimu Msingi pamoja na Elimu Sekondari. Ndg. Magaro pia aliweza kuwashukuru Waheshimiwa Madiwani waliokuwa masimamizi wakuu kwenye Kata husika kwa kusimamia kikamilifu miradi hiyo ambayo imekuwa na tija kwa wananchi.
Kwa upande wake, aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Charles Kazungu amesema Serikali chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa kwenye kuleta maendeleo kwa wananchi, pamoja na kufungua milango ya fursa kwa wafanyabiashara, huku akitoa msisitizo wa Halmashauri kuendelea na kasi ya ukusanyaji wa mapato ili lengo la bajeti iliyopangwa, liweze kufikiwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa