July 25 kila mwaka ni siku ya Historia kwa taifa la Tanzania ambapo huadhimisha siku ya kumbukumbu ya mashujaa katika kuwaenzi mashujaa ambao kwa uzalendo mkubwa na ujasiri wao waliweza kujitolea maisha yao kwa ajili ya taifa letu katika kupigania uhuru na kuilinda nchi yetu.
Tunapoadhimisha siku hii, tunatambua na kuthamini juhudi zao katika kuleta amani uhuru na maendeleo katika taifa letu. Siku ya mashujaa inatupa fursa ya kujifunza kutokana na historia yetu na kufahamu umuhimu wa kuwa na moyo wa kujitolea kwa ajili yawengine.
Tunawaenzi mashujaa wetu kwa matendo yetu ya kila siku kwa kufanya kazi kwa bidii, kufanya matendo ya kijamii ikiwa ni pamoja na kufanya usafii kwenye hospitali, nyumba za wazee, kupanda miti, kuendelea kuilinda amani na kushirikiana kwa hali na mali kwa maendeleo ya taifa letu.
Katika kuadhimisha siku hii muhimu kwa taifa letu, watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndg Karia Rajab Magaro leo Julai 25, 2024 wameshiriki zoezi la usafi katika hospitali ya Wilaya-Nzera pamoja na kupanda miti.
Mkurugenzi Mtendaji ndg Karia Rajab Magaro akipanda mti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mashujaa Tanzania ambapo kila mwaka huadhimishwa Julai 25.
Akizungumza na watumishi mara baada ya zoezi la usafi na upandaji miti, Ndg Karia amewataka watumishi kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika kuendeleza na kulinda urithi wa mashujaa wetu na kuhakikisha vizazi vijavyo vinaishi katika taifa lenye amani na ustawi ili waendelee kuwa na kumbukumbu ya mashujaa waliopiginania nchi yetu.
Mkurugenzi Mtendaji ndg Karia Rajab Magaro akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Julai 25 katika siku ya kumbukumbu ya maadhimisho ya siku ya mashujaa Tanzania ambapo siku hii ni katika kutambua na kuthamini juhudi za Mashujaa katika kuleta amani uhuru na maendeleo katika taifa letu.
Aidha kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika katika jiji la Dodoma ambapo mgeni rasmi ni Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakiwa katika zoezi la usafi katika siku ya kumbukumbu ya maadhimisho ya siku ya mashujaa Tanzania.
Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg Hendrick Msangi akipanda mti katika siku ya kumbukumbu ya maadhimisho ya siku ya mashujaa ambayo huadhimishwa kila mwaka Julai 25.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa