Nzera-Geita, Agosti 30, 2024
Kila mwaka Serikali inatumia sehemu kubwa ya fedha zinazoidhinishwa kwenye bajeti za Mafungu mbalimbali kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa, kandarasi za ujenzi na huduma kwa kuzingatia matakwa ya sheria ya ununuzi wa umma, SURA 410 na kanuni zake.
Aidha serikali imeendelea kudhibiti matumizi ya fedha zinazopolekwa kwenye kila fungu kwa kutumia njia mbalimbali ikiwepo mifumo ya kielekroniki ili kuleta tija na ufanisi unaostahili katika utekelezaji wa bajeti ya fungu husika.
Mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kielekroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) yameendelea kutolewa kila mara ili taasisi nunuzi zote ziweze kutumia mfumo wa NeST pamoja na watumishi wa umma wote wanaohusika na mchakato wa manunuzi ndani ya Taasisi kuwa na uwezo wa kutumia mfumo huo baada ya kuandaa bajeti sahihi inayo akisi ununuzi halisi unaofanyika kwa kila idara ndani ya taasisi hizo.
Katika kuhakikisha matumizi ya mfumo wa manunuzi wa NeST unatumiwa ipasavyo, Halmashauri ya Wilaya ya Geita kupitia Idara zake imeendelea kutoa mafunzo ili kuwajengea uwezo watumishi wa umma kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo wa NeST.
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bi Sarah Yohana Yohana amewataka watumishi wa umma kuzingatia kanuni za manunuzi ili fedha iliyoletwa na serikali iweze kukamilisha miradi lengwa na kwa wakati. Ameyasema hayo Agosti 30, 2024 akifungua mafunzo ya matumizi ya mfumo wa manunuzi wa umma NeST yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Awali akifungua mafunzo kwa watumishi wa umma wenye miradi katika maeneo yao ,Walimu Wakuu, Wahasibu wa shule na Maafisa elimu kata wa shule za msingi Ikigijo iliyopo kata ya Kakubilo na Bwawani kata ya Ludete zilizopokea fedha za miradi Shilingi Milioni 348,500,000 kila moja, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bi Sarah Yohana amewataka watumishi hao kuzingatia kanuni za manunuzi ili fedha iliyoletwa na serikali iweze kukamilisha miradi lengwa na kwa wakati.
Aidha Bi Sarah Yohana amewata watumishi hao kusimamia matumizi sahihi ya BOQ na kusisitiza manunuzi yote yazingatie bei ya soko na ubora wa vifaa kwa mujibu wa BOQ au makisio pamoja na kuwa na faili la mradi (Box file) ili kila nyaraka ya mradi ihifadhiwe kwa mpangilio ikiwemo mikataba watakayoingia na mafundi.
Watumishi wa umma ambao ni wasimamizi wa miradi katika maeneo yao ,Walimu Wakuu, Wahasibu wa shule na Maafisa elimu kata wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri wakati wa mafunzo ya mfumo wa manunuzi wa umma NeST. Katika mafunzo hayo wamesisitizwa kusimamia matumizi sahihi ya BOQ na kusisitiza manunuzi yote yazingatie bei ya soko na ubora wa vifaa kwa mujibu wa BOQ au makisio pamoja na kuwa na faili la mradi (Box file) ili kila nyaraka ya mradi ihifadhiwe kwa mpangilio ikiwemo mikataba watakayoingia na mafundi.
Kwa upande wake Mkuu wa divisheni ya elimu ya awali na msingi Mwl Paul Magubiki amewasisitiza walimu hao kuzingatia maelekezo yaliyotolewa katika mafunzo hayo ili miradi iweze kukamilika kwa wakati na kuwataka kubainisha mapema changamoto watakazokuwa wanapitia na kuziwasilisha kwa wakati ili taasisi iendelee kusimamia sheria za manunuzi na kuwataka kukubali mabadiliko ya kimfumo.
Jumla ya kiasi cha shilingi milioni 697,000,000 zimepokelewa kwa ajili ya miradi ya shule mbili za msingi ambazo ni Ikigijo iliyopo kata ya Kakubiro jumla ya shilingi 348,500,000 na shule ya msingi Bwawani kata ya Katoro shilingi 348,500,000.
Mkuu wa divisheni ya elimu ya awali na msingi Mwl Paul Magubiki amewasisitiza walimu wanaosimamia miradi katika maeneo yao kuzingatia maelekezo yaliyotolewa katika mafunzo ya mfumo wa manunuzi wa umma NeST ili miradi iweze kukamilika kwa wakati na kuwataka kubainisha mapema changamoto watakazokuwa wanapitia na kuziwasilisha kwa wakati ili taasisi iendelee kusimamia sheria za manunuzi
Halmashauri ya Wilaya ya Geita inaendelea kuishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika kuwatumikia wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa