Na: Hendrick Msangi
KAMENA MAY 19, 2024
Kazi imeendelea ikiwa ni operesheni ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi katika Kata 9 za awamu ya kwanza Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Akiwa katika kata ya Kamena inayoongozwa na Diwani Mhe Peter Kurwa, Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Komba amekagua miradi ya maendeleo ambayo ni zahanati, nyumba za watumishi na ujenzi wa shule katika vijiji vinne katika kata hiyo ambavyo ni Kamena, Nyashihima, Imalampaka na Ndelema.
Mhe Hashim Abdallah Komba wa kwanza kushoto, Mkuu wa Wilaya ya Geita akiwa na Kaimu Katibu Tawala Janet Mobe, pichani kulia, wakiwa wamebeba tofari alipotembelea ujenzi wa Shule ya Sekondari yenye vyumba 3 vya madarasa Kijiji cha Ndelema kata ya Kamena nguvu za Wananchi ambapo alifanya harambee ndogo na kupatikana mifuko ya saruji 200 katika kuunga mkono juhudi za Wananchi.
Akimkaribisha katika kata hiyo, Mhe Winfrida Daudi Malunde ambaye ni diwani wa viti maalum na mlezi wa kata hiyo, amemuomba mkuu wa wilaya ya Geita, kupitia CSR kuweka mkazo miradi ya afya katika kata hiyo ili kuendelea kuwapunguzia wananchi umbali mrefu kupata huduma za afya. “Umeminiwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, tunaamini hakuna kazi itakayosimama, tunaomba kupitia Mgodi wa Dhahabu (GGML) fedha za CSR zikakamilishe miradi ili wananchi wapate huduma katika maeneo yao. Amesema Mhe Winfrida Malunde diwani mlezi wa kata ya Kemana
Kiongozi ni mfano. Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba amewataka Watumishi kuendelea kusimamia fedha za wananchi zinazokuja kwenye maeneo yao kwa uadilifu mkubwa sana, "sitavumilia kuona fedha za wananchi zinachezewa, hivyo mkasimamie fedha za miradi zinazokuja katika maeneo yenu”
Akihutubia Mkutano wa Hadhara katika kusikiliza kero za wananchi, Mhe Komba amesema hatovumilia kuona fedha za wananchi zikichezewa na miradi ikishindwa kukamilika na kuwataka watumishi wa umma kusimamia fedha ili miradi iende vizuri. “Endeleni kusimamia fedha za wananchi zinazokuja kwenye maeneo yenu kwa uadilifu mkubwa sana, sitavumilia kuona fedha za wananchi zinachezewa, hivyo mkasimamie fedha za miradi zinazokuja katika maeneo yenu” amesema Mhe Komba.
Aidha Mhe Komba ametoa pongezi kwa jitihada zilizoanza kufanywa na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) kupitia fedha za wajibu wa kampuni kwa jamii (CSR) kwa kupeleka wakandarasi na kuanza haraka kwa ukamilishaji wa mradi wa ujenzi wa vyumba sita vya madarasa katika shule ya msingi Kamenaikiwa ni siku chache tangu alivyoitisha kikao na wadau hao katika kuweka makabaliano ya kukamilisha miradi na kuwataka wale wote wanaohusika na miradi ya maendeleo kuacha uzembe ili wananchi wasiendelee kuteseka.
Ukamilishwaji wa Madarasa 7 shule ya Msingi Kamena unaotekelezwa na Kampuni ya Gesap Engineering Ltd.
Pamoja na hayo ameendelea kusisitiza uwepo wa madawati ya kusikiliza kero za wananchi kwa kushuka chini kusikiliza wananchi na sio kukaa ofisini. “Nimekuja mwenyewe kuonyesha mfano ili kusikiliza kero na changamoto za wananchi na nimeambatana na wataalam wa kada zote ili kuisogeza serikali jirani na wananchi
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa