Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita John Paul Wanga,amewaagiza watendaji wa kata zote kuandaa kanzi data ya wakulima na mazao yao wanayozalisha, ili Halmashauri ipate takwimu sahihi na kuandaa utaratibu mzuri wa kuwasaidia katika kupata pembejeo bora za kilimo,na kuongeza uzalishaji.
Ameyasema hayo Agosti 20 alipokutana na watendaji wa kata zote na wakuu wa idara za Halmashauri ya walaya ya Geita ambapo amesema kuwa,ni rahisi zaidi kuwahudumia watu ukiwa na takwimu sahihi ya idadi yao na kile wanachokifanya,huku akiwaagiza watendaji hao wa kata kufanya usajili wa kila mkulima na zao analozalisha ili kuwasogezea huduma,waongeze uzalishaji,wajipatie fedha na hatimaye kuongeza mapato ya Hamshauri.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita akiongea na wakuu wa idara na watendaji wa kata katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita
Aidha baada ya kupata idadi ya kata ambazo zinalima alizeti,amemuagiza mkuu wa idara ya kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bw.Daud Lutema, kuhakikisha anafuatilia mbegu bora za zao hilo na kuzipeleka kwa wakulima ili wahamasike zaidi na kilimo hicho.
Wakati huohuo amewataka watumishi wa idara mbalimbali kufanya kazi kwa kujituma ili kuwasaidia wananchi kupata huduma bora,ambapo ameeleza kuwa hawezi kuwavumilia watumishi wazembe,akitumia kauli yake ya "watumishi ni marafiki zangu,lakini ni adui wa watumishi wazembe na wabadhilifu".
Picha ya pamoja kati ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita John Paul Wanga akiwa na watendaji wa kata mara baada ya kikao
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa