WASIMAMIZI WASAIDIZI wa Uchaguzi ngazi ya Kata Halmashauri ya Wilaya ya Geita Leo Agosti 04,2025 Wamepewa Mafunzo kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025. Mafunzo hayo yamefanyika Katika Ukumbi wa Halmashauri Uliopo Bomani Geita Mjini.
Akifungua Mafunzo hayo, Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bi Sarah Yohana amewapongeza Wasimamizi hao kwa Kuchaguliwa na Tume Huru ya Taifa kwa Mujibu wa Masharti ya Kifungu cha 6(2), cha sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na.1 ya Mwaka 2024 kwa kuzingatia Utendaji wenye Uadilifu, Uaminifu, Uzalendo na Uchapakazi.
Pamoja na Pongezi hizo Bi Sarah Yohana amewataka wasimamizi hao kuzingatia Katiba, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ,Mkajiepusha Kuwa Vyanzo vya Malalamiko Kutoka kwa Vyama vya Siasa na Wadau wa Uchaguzi” Amesema Bi Sarah.
Vilevile Msimamizi huyo wa Uchaguzi Ngazi ya Halmashauri ameendelea kuwaasa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata Kuwashirikisha Wadau wa Uchaguzi hususani katika maeneo ambayo kwa Mujibu wa Katiba, Sheria, Kanuni, Miongozo na Maelekezo yatakayotolewa na Tume ambayo Wanastahili Kushirikishwa.
Aidha Bi Saraha amewasisitiza Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata Kufanya Utambuzi wa Vituo vya Kupiga Kura Mapema ili Kubaini Mahitaji Maalum ya Vituo Husika na Kuhakikisha Kuna kuwa na Mpangilio mzuri utakao ruhusu Uchaguzi kufanyika kwa Utulivu na Amani ikiwa ni Pamoja na Kuvishirikisha Vyama vyote vya Siasa Vyenye Usajili Kamili Katika Hatua Zote kwa Kuzingatia Matakwa ya Katiba, Sheria, Kanuni na Maelekezo Mbalimbali ya Tume.
Akihitimisha Hotuba yake katika Mafunzo hayo ambayo yamejumuisha Washiriki 74 kutoka Kata 37 za Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambao ni wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata amewataka Wasimamizi hao Kuwajibika ipasavyo.
“Mnategemewa Kuzingatia utendaji wenu, muwajibike ipasavyo katika kipindi chote cha Utumishi wenu kwa Tume hadi hapo tutakapokamilisha jukumu hili la Uchaguzi.”Ameongeza Bi Sarah Yohana.
Kwa Upande wake Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Geita Ndg Matemu amewataka Wasimamizi hao kujiepusha na Vitendo vya Upendeleo vitakavyo kwamisha zoezi la Uchaguzi kuwa la Huru na la Haki.
Mafunzo hayo yanaongozwa na Kauli mbiu isemayo; Kura yako Haki yako Jitokeze Kupiga Kura yanatarajiwa kufanyika kwa Siku tatu ambapo yatahitimishwa Agosti 06, 2025.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa