• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

WASIMAMIZI WASAIDIZI 145 NGAZI YA VIJIJI WAPEWA MAFUNZO KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Posted on: October 2nd, 2024

Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa ngazi ya vijiji wapatao 145 wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita wameapishwa leo Oktoba 2, 2024.

Uapisho huo umeongozwa na Muchunguzi Mujuni Sailous Hakimu Mkazi Mwandamizi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita zamani-Bomani.

Wasimamizi Wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Vijiji Wakiapa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Muchunguzi Sailous Leo Oktoba 2, 2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita zamani-Bomani

Pamoja na zoezi la kuapishwa, wasimamizi wasaidizi hao wamepewa mafunzo kuhusu namna watakavyotekeleza majukumu yao kabla, wakati na baada ya zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa.

Katika ufafanuzi wake kwa wasimamizi Wasaidizi hao, Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Amina Sungura amesema zoezi hilo linaongozwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Kanuni za uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji na vitongoji katika Mamlaka ya Wilaya ya Mwaka 2024.

Amewataka wasimamizi kuzingatia muongo katika kazi yao ikiwemo kutokuwa viongozi wa vyama vya siasa, kuwa Watiifu na Waadilifu, Waaminifu na kutunza siri.

Pichani wa kwanza Kushoto ni Mwanasheria Amina Sungura, Aliyekaa katikati ni Afisa Msimamizi Msaidizi Jonas Kilave na wa kwanza kulia ni Afisa Msimamizi Msaidizi  Sarah Yohana ngazi ya Halmashauri

Kuhusu sifa za mpiga kura Mwanasheria Sungura,  amesema kuwa  mpiga kura lazima awe Mtanzania mwenye  umri wa miaka 18 na kuendelea, awe mkazi wa mtaa,kijiji au kitongoji anapoishi, awe na akili timamu na awe amejiandikisha katika kitabu cha mpiga kura katika mtaa,kijiji au kitongoji  husika.

Naye Afisa Msimamizi msaidizi Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bi Sarah Yohana  amewataka wasimamizi wasaidizi kuwa makini na zoezi hilo kwa kuwa wamepewa dhamana ya kufanya kazi hiyo kwasababu wameaminiwa hivyo wafanye kazi na kuikamilisha kama ilivyokusudiwa.

Afisa Msimamizi Msaidizi Bi. Sarah Yohana akitoa maelekezo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Vijiji katika mafunzo yaliyofanyika Bomani Geita Mjini Leo Oktoba 2, 2024.

Akihitimisha mafunzo hayo Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg Karia Rajabu Magaro amewatangazia wasimamizi wasaidizi kwamba tarehe ya uandikishaji wapiga kura ni Oktoba 11 hadi 20, 2024 hivyo wahakikishe kwamba unafanyika kama unavyostahili.

Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndugu Karia Rajabu Magaro akitoa maelekezo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Vijiji katika Ukumbi wa Mikutano Bomani Geita Mjini Leo Oktoba 2, 2024

Amewataka wasimaizi wasaidizi kudumu katika maeneo yao ya kazi na kwamba kama kuna sintofahamu yoyote wanapaswa kutoa taarifa kwa  Afisa uchaguzi au Msimamizi wa Uchaguzi.

Amesema pia hatosita kumchukulia hatua msimamizi msaidizi ngazi ya kijiji yeyote atakaeshindwa kutekeleza wajibu wake vizuri hivyo kila mmoja afanye kazi hiyo  kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa.

Lameck  Warioba msimamizi msaidizi wa uchaguzi  ambaye ni Afisa mtendaji  kijiji cha Ikina kata ya Bukoli Wilaya ya Geita, amesema amepokea mafunzo hayo kwa umakini na anaahidi kwenda kusimamia zoezi hilo kwa haki na kwa kuzingatia misingi, kanuni na taratibu zilizotolewa.  

Wasimamizi  Wasaidizi  wa uchaguzi ngazi ya Vijiji wakijaza fomu za viapo Oktoba 2, 2024 kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO KWA VIKUNDI January 23, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RUSHWA NI JANGA LINALOATHIRI MAENDELEO YA KIUCHUMI, KIJAMII NA KISIASA NCHINI-RAS GOMBATI.

    May 13, 2025
  • GEITA YAPATA MAJIMBO MAPYA YA UCHAGUZI.

    May 12, 2025
  • ALAT MKOA WA GEITA WAMPONGEZA MKURUGENZI GEITA DC USIMAMIZI MZURI WA MIRADI

    May 10, 2025
  • UBORESHAJIWA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025 WAFIKIA KIKOMO GEITA.

    May 08, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa