Na Hendrick Msangi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ihumilo kata ya Nkome Halmashauri ya Wilaya ya Geita ndugu Tumaini Christopher ameiomba Serikali kupeleka askari wa usalama barabarani kwenye kituo cha mabasi Ihumilo ambacho hakifanyi kazi kwa sasa Licha ya kuwa na miundombinu yote inayohitajika katika kituo hicho.
Hayo yameelezwa Novemba 7, 2023 wakati timu ya utawala (CMT) ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita ikiongozwa na Mkurugenzi wake Ndugu Karia Rajabu Magaro ilipotembelea kituo hicho cha mabasi kwenye kata hiyo ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kutembelea miradi inayoendelea kwenye Halmashauri hiyo.
Timu ya utawala (CMT) ikiongozwa na Mkurugenzi wake Ndugu Karia Rajabu Magaro walipotembelea kituo cha mabasi Ihumilo kata ya Nkome.
Kituo hicho cha mabasi kilianza kutumika Januari 03, 2020 lakini baadaye kilisimama kufanya kazi kwani magari licha ya kuwa na jengo la kupumzika abiria, huduma za choo, kituo kidogo cha kukaa askari polisi lakini magari hayafi kituoni jambo ambalo linafanya mradi huo kuharibiwa miundombinu yake.
" Tunamuomba Mhe Diwani kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanya hamasa ya kuendeleza kituo ili magari yaweze kufika na ushuru ukusanywe eneo la kituo cha mabasi kwani kwa sasa anayekusanya ushuru analazimika kuyafuata magari sehemu ambayo sio kituo sahihi" alisema Mwenyekiti Huyo.
Akiongoza timu hiyo Mkurugenzi Magaro aliwataka Viongozi hao wa serikali ya kijiji na kata kuchukua hatua madhubuti ili kituo hicho cha mabasi kiendelee kufanya kazi kama ilivyo kuwa awali.
" Fanyeni usafi wa kituo hiki kuyatunza mazingira na miundombinu yake ambayo inaharibiwa kutokana na kituo cha mabasi kutokufanya kazi, " alisema Magaro.
Pamoja na ziara katika kituo hicho cha mabasi, timu hiyo iliweza kutembelea mradi wa kituo cha afya Nkome wenye jengo la OPD, maabara na jengo la Upasuaji ambapo fedha za mradi huo ni jumla ya kiasi cha shilingi milioni miatano ( 500,000,000) kutoka CSR.
Mradi wa Kituo cha afya kata ya Nkome unaotekelezwa kwa fedha za CSR kiasi cha shilingi 500,000,000.
Mkurugenzi aliwataka wakandarasi wanaotekeleza mradi huo kuongeza kasi kwa kuwa fedha za mradi zipo.
"Kazi zifanyike kwa wakati kwani Serikali imekwisha tenga fedha za mradi zipo hakuna sababu ya kuchelewesha ukamilishwaji wa mradi huu" alisema Magaro.
CMT wakikagua mradi wa wa kituo cha afya Nkome. Mkurugenzi alitoa maagizo kwa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo kuongeza kasi na kuhakikisha kuna Kuwa na mafundi wa kutosha ili kazi ifanyike kwa uharaka.
Mradi huo kwa mujibu wa mkataba wake unatarajiwa kukamilika Desemba 30,2023 ili wananchi waweze kupata huduma.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita inaendelea kuishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuipatia fedha nyingi kukamilisha miradi mbalimbali na kuleta maendeleo kwa Watanzania.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa