Nzera, Geita.
Wananchi Wilayani Geita wamehimizwa kujiunga kwenye Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili waweze kupata huduma za afya kwa urahisi na kwa gharama nafuu.
Akizungumza hii leo Aprili 30, mbele ya Baraza la Madiwani katika ukumbi wa Halmashauri kwenye kikao cha uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Robo ya Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, Meneja Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoa wa Geita, Bw. Elias Odhiambo amewasihi wananchi kujiunga kwenye mfuko huo kutokana na fursa za uanachama zinazopatikana.
Bw Odhiambo pia amezungumzia huduma ya Mifumo ya Kielektroniki ya kujihudumia (NHIF Self Services) ambayo inatolewa na mfuko huo inayojumuisha vifurushi na vitita mbalimbali ambayo wananchi wanaweza kujiunga navyo na kupata huduma popote pale.
Kwa upande mwingine, Bw. Odhiambo ameiomba Halmashauri ya Geita kuiweka ajenda ya Bima kwa wote iwe ajenda ya kudumu ya kujadiliwa katika vikao vya Mabaraza ya Madiwani, kutoa taarifa sahihi pindi watakapoanza zoezi la kusajili kaya zisizojiweza ili wananchi waweze kupata huduma ya Bima, pamoja na kutoa elimu kwa Wananchi waweze kuona umuhimu wa kujiunga na mfuko huo.
Huduma ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unalenga sekta zote rasmi na sekta zisizo rasmi ili wananchi wote waweze kupata huduma kulingana na uwezo wao wa kugharamia vifurushi vinavyotolewa na mfuko huo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa