Mkuu wa wilaya ya Geita Mh. Wilson Shimo amempongeza Rais Samia suluhu Hasan kwa jitihada kubwa alizoziweka katika kuhudumuia wananchi wa Tanzania kupitia sekta ya afya.
Mheshimiwa Wilson Shimo Amesema hayo kwenye zoezi la ukabidhianaji wa Boti ya kisasa iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita wanaoishi maeneo ya visiwani.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Edith Mpinzile amekabidhiwa rasmi boti hiyo ya kisasa na watumishi wa TASAC na TEMESA leo Agosti nne 2021 na kushuhdiwa na Mkuu wa Wilaya Mh Wilson shimo.
Aidha Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dr. Modesti Rwakaemula amesema Boti hiyo imegarimu fedha shilingi 236 milioni na ina kila huduma inayohitajika katika afya kabla mgonjwa hajafikishwa Hospitalini na kwamba itatumika kuwabeba wakinamama wajawazito,watoto chini ya miaka mitano pamoja na wazee wenye umri zaidi ya miaka 60.
Kwa wagonjwa wengine watalazimika kuchangia kiasi kidogo kwa ajili ya mafuta.
Kwa upande wa wananchi wa Kata ya Nkome wemepongeza jitihada zilizofanywa na serikali kwa kuwapelekea Boti hiyo na kwamba itaondoa changanoto ya wakinamama kujifungulia kwenye mtimbwi na wengine kupoteza maisha.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa