LISHE ni jambo ambalo Limepewa kipaumbele kikubwa na Serikali ya awamu ya Sita inayo ongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika kuunga Juhudi za Serikali kutekeleza afua za Lishe, Januari 30,2025 maafisa Lishe kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita wametembelea Kisiwa cha Izumacheli kilichopo ziwa Viktoria kwa ajili ya kutoa elimu ya Lishe kwa wananchi kisiwani humo.
Akizungumza katika Mafunzo hayo Afisa Lishe Bi Nasim Ginga amesema lengo kuu la wao kutembelea kisiwani Izumacheli ni kutoa elimu ya namna ya kuandaa chakula bora kilichozingatia makundi yote ya chakula pamoja na kutathimini hali ya Lishe ipoje ukanda wa Kisiwa cha Izumacheli.
Wananchi hao wameelekezwa kuandaa uji wa Lishe kwa kuzingatia upatikanaji wa vyakula vinavyopatikana katika mazingira yao.
Kwa upande wake Mapembe Gamva ambaye ni mkazi wa Izumacheli amesema Elimu hiyo ni muhimu sana kwao katika kusaidia watoto kupata Lishe bora kwa ajili ya ustawi wa afya zao.
Halikadhika Ndg Chuga Nistasi amesema ataitumia elimu hiyo kumuelekeza mke wake namna ya kuandaa Uji wa Lishe kwa kuzingatia upatikanaji wa vyakula vinavyopatikana katika Kisiwa hicho.
Naye Bi Zena Lawson (27) mkazi wa Kata ya Izumacheli ni mwanamke mwenye watoto wa tano ambapo ameishukuru Serikali kwa namna ambavyo inawajali wananchi waishio visiwani kwa kuwapatia elimu ya maswala ya Lishe.
Akihitimisha zoezi la utoaji wa elimu ya Afua za Lishe, Bi Ummy Kileo, Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Geita amesema zoezi hilo litaendelea kufanyika mara kwa mara katika Kisiwa hicho.
Makundi ya Vyakula ambavyo wananchi wameshauriwa kula ni pamoja na vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi za kupika, Vyakula vya asili ya wanyama, vyakula vya jamii ya mikunde, mbogamboga, Matunda, mafuta na maji ambayo sio kundi la chakula lakini ni muhimu sana kwa afya.
Wananchi Kisiwani Izumacheli wakielekezwa namna ya kuandaa uji wa lishe kwa kutumia mahitaji yanayopatikana katika mazingira yao
Afisa Lishe Bi Ummy Kileo akimuhudumia Mwananchi katika Kisiwa cha Izumacheli walipotembelea kutoa elimu ya afua za Lishe katika kata hiyo iliyopo kisiwani
Maafisa Lishe Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita Wakiwahudumia Wananchi wa Kata ya Izumacheli walipowatembelea kutoa mafunzo ya Afua za Lishe
Mtendaji wa Kata ya Izumacheli, Alfred Conrad akiwamiminia uji wa lishe wananchi waliojitokeza katika mafunzo hayo
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa