Timu ya wanamichezo kutoka Halmashauri ya Wilaya, Geita, hii leo Agosti 12, 2025 inatarajiwa kuanza safari kuelekea Jijini Tanga kushiriki mashindano yaliyoandaliwa na Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa, maarufu kama SHIMISEMITA.

Akizungumza na wachezaji hao mapema wiki hii ambapo alipata nafasi na kuhudhuria mazoezi ya timu hiyo katika viwanja vya Shule ya Sekondari, Katoro, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Ndg. Karia Magaro amewasisitiza wachezaji hao kuhakikisha wanajituma ili waweze kufanya vizuri pindi mashindano hayo yatakapoanza.

Naye Afisa Michezo Msaidizi Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Saguda Maduhu amesema kuwa maandalizi yameenda vyema na kwamba wachezaji wote wapo salama na wana ari ya kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

Jumla ya wanamichezo 59 wakijumuisha wanaume pamoja na wanawake, wanatarajiwa kuelekea Jijini Tanga kwenye mashindano hayo ambapo timu hiyo itashiriki kwenye Mchezo wa Soka, Wavu, Mpira wa Mikono, Mbio za Riadha, Mchezo wa pool, Bao, Karata na Mchezo wa Drafti.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi mnamo Agosti 15 yakijumuisha Halmashauri 184, ambapo kwa upande wa Soka, Halmashauri ya Wilaya ya Geita itashiriki kama bingwa mtetezi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa