Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim Komba, amewapongeza Walimu wilayani humo kwa kuchochea hali ya ufaulu miongoni mwa wanafunzi ambapo ufaulu umekua ukiongezeka haswa kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni, huku kwa mwaka 2025, shule 115 kati ya 227 Wilayani Geita zimeongeza ufaulu.
Akizungumza Disemba 19 na walimu hao kwenye hafla ya utoaji wa zawadi kwa shule zilizofanya vizuri kwenye mtihani wa Darasa la 7 2025, katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Aloysius, Ndg. Komba ameongeza kwa kusema kuwa walimu wameendelea kuwa mstari wa mbele kwenye kulisaidia taifa kwenye suala la ukuzaji wa malezi ya watoto.
Aidha, Mhe. Komba pia ameiagiza Idara ya Elimu Msingi kutengeneza programu maalum ya kuchochea ubunifu kwenye sekta ya elimu pamoja na kuandaa mpango kazi utakaoshirikisha walimu na wazazi ili kukuza ufaulu kwenye shule za msingi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Jumanne Misungwi amewataka walimu kudumisha somo la uzalendo kwa wanafunzi pamoja na kuwahimiza kudumisha Upendo na umoja miongoni mwao.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa