Na: Hendrick Msangi
Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita leo Novemba 21, 2023 wamepata mafunzo jinsi ya kutumia mfumo wa tathmini ya mahitaji ya rasilimaliwatu katika utumishi wa umma (HR Assessment System) kutoka kwa wataalamu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakifuatilia mafunzo jinsi ya kutumia mfumo wa tathmini ya mahitaji ya rasilimaliwatu katika utumishi wa umma (HR Assessment System)
Mfumo huo utatumika katika kuchakata mahitaji ya watumishi katika taasisi za umma ambapo utatoa takwimu sahihi kuhusu idadi ya watumishi waliopo, wapo wapi na mahitaji ya watumishi kwa ujumla ili kuisadia serikali katika kufanya maamuzi mbalimbali.
Aidha mfumo huo utaweza kukokotoa mahitaji ya rasilimali watu kwa kuangalia uwiano na uzito wa majukumu ya watumishi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwenye taasisi zao.
Awali mfumo uliokuwa ukitumika wa Joblist form katika kuchambua mahitaji ya rasilimaliwatu ulikuwa ukitumia njia ya majadiliano hivyo kuchangia matokeo yasiyokuwa na uhalisia ambapo kumepelekea malalamiko kutoka kwa waajiri juu ya upungufu/uhaba wa watumishi, kukosekana kwa takwimu sahihi zinazotumiwa na waajiri katika kuandaa maombi ya ajira pamoja na kukosekana kwa msawazo ulio sawa kwa watumishi hasa maeneo ya vijijini na mijini.
Mfumo wa tathmini ya mahitaji ya rasilimaliwatu katika utumishi wa umma (HR assessment system) utaiwezesha serikali kuwa na taarifa sahihi za watumishi waliopo na wanaohitajika, kufanya msawazo wa watumishi kwenye maeneo waliyozidi na maeneo yenye upungufu ikiwa ni pamoja na kuleta ufanisi na tija katika utumishi wa umma kwa kuisadia serikali kupanga mipango ya muda mfupi na muda mrefu juu ya Rasilimaliwatu
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa