Waandishi wa habari mkoani Geita watajwa kama kundi la kwanza, lenye wajibu wa kupeleka elimu sahihi kwa jamii ya kujikinga na janga la korona, na kuhamasisha chanjo ili kupunguza hatari zaidi.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mh.Wilson Samwel Shimo, wakati akifunga mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari, yenye lengo la kutoa elimu ya kujikinga na kukabiliana na Korona,yaliyotolewa na Idara ya Afya Mkoani Geita kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML).
Mh.Shimo amesema kuwa watu hawana elimu sahihi, hivyo kwa kuwaelimisha Wanahabari ni dhahiri kuwa, uelewa utaongezeka na wao kama Serikali ya Mkoa wanategemea kuona matokeo makubwa yaliyo mazuri.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini mafunzo waliyokuwa wakipatiwa kuhusu Korona.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Kampuni ya GGML Bw.Saimon Shayo amesema kuwa,wao kama mgodi wanatambua athari za janga hili la Korona na wanachukua hatua mbalimbali za kukabiliana nalo, sambamba na kufadhili miradi mbalimbali kama vile mitungi ya oksijeni kwa wenye matatizo ya kupumua,vifaa tiba, na vifaa vya kutakasa mikono sehemu zenye mikusanyiko.
Awali akitoa mafunzo hayo kwa Wanahabari Wille Luhangija ambaye ni Afisa Afya anayeratibu chanjo Mkoa wa Geita amesema kuwa, mwitikio wa chanjo ya Korona Mkoani hapa ni mdogo kuliko sehemu yoyote hapa nchini, ambapo tangu kuzinduliwa kwa chanjo hiyo takwimu zinaonyesha ni 10% pekee ya wananchi ndio waliochanjwa mpaka sasa.
Wille Luhangija Mratibu wa chanjo Mkoa wa Geita akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu Chanjo ya Korona
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa