Viongozi wa Serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Geita ambao wameapishwa Novemba 28 wameahidi kupigania maendeleo ya elimu katika maeneo yao ya utawala
Baadhi ya viongozi hao wakiwemo Suzana Buganda ambaye mwenyekiti wa Sungusila na Sobolwa John ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha Likelege wametaja changamoto mbalimbali za elimu katika maeneo yao zinazotakiwa kutatuliwa
Viongozi hao ni miongoni mwa viongozi wengine 221 kutoka tarafa za Kasamwa na Bugando katika halmashauri wilaya ya Geita ambao wameapishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya mwanzo Sabato Bwire huko Nzera
Mkuu wa wilaya ya Geita, Josephat Maganga ambae alikuwa mageni rasmi katika uapishaji huo amewataka viongozi hao kusimamia haki na kufanya kazi bila ubaguzi wowote ule
Awali kabla ya zoezi la uapishaji aliekuwa msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mtaa Halmashauri ya wilaya ya Geita ,ndugu Dornald Nsoko katika taarifa yake ameeleza kuwa jumla ya wapiga kura 221506 waliandikishwa kati ya 3470077 sawa na 63.8% ya lengo la uandikishaji.
Viongozi hao waliyoapishwa ni wale waliyoshinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliyofanyika November 24 mwaka huu.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa