Vijana Wilayani Geita wanatarajiwa kupatiwa suluhu ya namna gani wanaweza kuzitambua fursa zinazowazunguka na kuzitumia ipasavyo ili kujiingizia kipato.
Akifungua kikao cha majadiliano ya utekelezaji wa mradi wa Bridge Tanzania Project mwishoni mwa juma katika Shule ya Msingi Nzera, mbele ya Maafisa Elimu Kata, Mratibu wa kitaifa wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, Bi. Fatma Mrope amesema kuwa mradi huo utawapa nafasi vijana, haswa Wanawake (Takriban 55%) kuzitambua changamoto zinazowakabili, na namna gani wanaweza kutumia stadi watakazozipata, kukabiliana nazo kwenye maeneo yao.
Mradi huo unaosimamiwa na Tume ya Taifa ya Shirika la UNESCO nchini, chini ya ufadhili wa Tume ya Taifa ya UNESCO nchini Korea; Korea National Commission for UNESCO (KNC-UNESCO), utalenga kuwafanya vijana waweze kujisimamia na utagusa sekta tofauti kama vile Kilimo, Uvuvi, pamoja na sekta ya Ufugaji, ambazo ni sekta zinazokua kwa kasi nchini.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa