Na: Hendrick Msangi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndugu Karia Rajabu Magaro Leo October 29, amezindua hotel ya The Giant iliyoko mji mdogo wa Katoro.
The Giant Hotel Katoro-Geita.
Akitoa hotuba yake kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Mh Martin Shigela, alimpongeza mmiliki wa hôtel hiyo mfanyabiashara Peter Semeni. " Mkuu wa Mkoa anakupongeza sana kwa kazi kubwa uliyoifanya kujenga hotel hii yenye hadhi kubwa na leo tunaizundua" Alisema Magaro.
Akiendelea kutoa hotuba yake, Mkurugenzi huyo alisema Mhe Rais anavutiwa na wawekezaji kama Mfanyabiashara huyo kwani kuwepo kwa hotel hiyo kumezalisha ajira kwa vijana jambo ambalo linaleta maendeleo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndugu Karia Rajabu Magaro akizindua hotel ya The Giant iliyoko mji mdogo wa Katoro. Kulia ni mmiliki wa hôtel hiyo mfanyabiashara Peter Semeni.
Pamoja na hayo, Mkurugenzi Magaro aliwasihi wakazi wa Katoro wawe tayari kuleta wageni kwenye hotel hiyo ili kumuunga mkono mmiliki huyo. " Tuna wajibu wa kuleta wageni wengi kwenye hotel ya The Giant na Serikali ipo tayari kuwaleta Viongozi kwani ni hotel yenye hadhi kubwa zikiwepo sehemu za kufanyia mikutano" alisema Magaro.
Aidha alimuhakikishia mmiliki huyo kuwa serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Geita ipo tayari kumsaidia atakapohitaji msaada ikiwa ni pamoja na wafanyabiasha wengine katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ili kuendelea kuleta maendeleo makubwa katika mkoa wa Geita.
The Giant hotel ni hotel ya kisasa iliyopo kata ya Ludete Wilayani Geita. Kuanza kazi kwa hotel hiyo kutaingizia Halmashauri mapato na kuendelea kuzalisha ajira nyingi kwa vijana mkoani Geita.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa