Nzera, Geita.
Tume ya Taifa ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kwa ufadhili wa Tume ya Taifa ya UNESCO ya nchini Korea, (KNC-UNESCO), imepanga kuwainua kiuchumi vijana Wilayani Geita waishio katika mazingira magumu pamoja na wale waliokosa nafasi ya kujiendeleza kimasomo kwa kupitia uanzishaji wa miradi endelevu itakayowawezesha vijana hao kujitegemea.
Akizungumza hii leo katika ofisi za Halmashauri na baadhi ya Maafisa kutoka Idara tofauti za Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Mratibu wa Mradi kitaifa wa UNESCO, Bi. Fatma Mrope amesema, lengo kuu la kuanzishwa kwa mradi huo ni kuhakikisha unawajengea uwezo vijana kwa kuwapatia mbinu za namna ya kuanzisha miradi mbali mbali ya kiuchumi ambayo vijana wataianzisha, kuisimamia, na kuiendesha ili waweze kujiingizia kipato.
Bi. Fatma ameongeza kwa kusema kuwa, Tume hiyo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Geita, itahakikisha vijana wanakutana na wakufunzi na wabobezi wa sekta mbali mbali ambao wataweza kuwapa maarifa stahiki yatakayowawezesha vijana kuyaendea masoko ya bidhaa na huduma ambazo watakua wamezianzisha.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa